NA MBEYA YETU
MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda, wamekutana leo Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu ikiwa na kuweka mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi. Mkutano huo unafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya usalama na uhalifu wa maeneo katika Mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma, Njombe na Mbeya . 
Akizungumzia mikakati hiyo, Mwenyekiti wa Mkutano Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile alisema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo. 

Amesema Wahalifu wamekuwa na tabia ya kuhama hama mara wanapofanya tukio, hawakai sehemu moja hivyo mkutano huu utasaidia kwa wajumbe kubadilishana na kupeana uzoefu wa kazi,’alisema Aidha, amefafanua kuwa jeshi la polisi hivi sasa kupitia baadhi ya askari limekuwa likikumbwa na matukio ya ukiukwaji wa maadili kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali za uhalifu. 
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , alisema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali barabarani. 
Amesema mara nyingi Wahalifu wamekuwa wakitumia njia nyingi kufanya uhalifu na kukimbilia mikoa ya jirani hivyo mkutano huu ambao unahudhuriwa na Makamanda pamoja na wakuu wa upelezi utasaidia kuwabaini ikiwa na kusambaratisha mtandao uliopo Mkutano huo ni watatu baada ya mkutano wa kwanza kufanyika Mkoani Iringa na wa pili ulifanyika Mkoani Morogoro na kwamba wajumbe wanatarajia kutoka na maadhimio mapya.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , amesema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali barabarani.

Mwenyekiti wa Mkutano  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile amesema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo.
Baadhi ya maafisa wa jeshi hila la Polisi wakiwa makini kusikiliza mwenyekiti wao katika kikao hicho
Baadhi ya makamanda wa polisi wakiwa maetulia kwa umakini kumsikiliza mwenyekiti wa kikao hicho
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2013

    Hivi haya mambo ya hawa polisi/ jeshi kuwa na vifimbo ndio nini? tuko karne ya 21 bado hatujaacha mambo ya kizamani ya kurithishwa na wakoloni? kwanza maana yake ni nini? ni kama vile akiingia spika wa bunge huja na watu wakiemskoti na rungu ,kama si ujinga ni kitu gani? na kwa nini apewe eskoti kwani yeye si binadamu kama wengine? 'kila mtu anastahili heshima' lakini mbona hapa kwetu TZ viongozi wanapewa utukufu badala ya heshima? kwani mtu akiwa mkubwa ni lazima aitwe mheshimiwa ? kwani kuna viongozi wengine waliodharauliwa ili kupambanua baina yao ?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2013

    Kaka yangu wee mtoa mada wa kwanza, hizo ni swags za watanzania, nishati nyingi inapotea lakini hakuna kinachofanyika. kuhusu hivyo vijiti wanavyojitwisha kila uchao ukiwauliza watakwambia mambo ya protocols na misemo yao wenyewe.Majasho meeengi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2013

    Vitambi kwa polisi noma nilishaona kwa macho yangu polisi walikuwa wamesimama nje ya kituo fulani akapita kibaka anakimbizwa na wananchi akakatiza kituoni katikati ya polisi 3 wakajipinduapindua pale kibaka huyooo!! mbio hawana akaishia Kweli Kitambi noma!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2013

    Jamani ila hawa kidogo wamejitahidi kutokua na mitambi mikubwa, work out guys ondoeni kabisa hivyo vitambi you are coming up fine du ila mmependeza na kutokuwa na mitumbo mikkuuuubwa na mtapendeza zaidi mkiwa slim kabisa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 22, 2013

    Hawana lolote! kazi kuuwa wananchi wasio na hatia, na kubambikiza watu kesi. Kila uhalifu unaojitokeza askali anakuwa nyuma yake.

    Msiwaone wamependeza wanasubiri hella ya mboga hao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 22, 2013

    hahahahaaaaa jamani ushamba umetuzidi Tanzania kwani lazima ukiwa kiongozi ujulikane kiongozi, inahuuuuuu, uongozi kwenu na ndugu zako cheo kinahusu familia yako, anoyy wa juu umeongea ukweli, tunaboa bwana bongo

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 22, 2013

    Hiyo ndiyo POLISI!

    MBEYA NA MAANDAMANO YA KISIASA (nyuma ya Paziz).

    Wakubwa Makamanda wa Polisi wamesha wasoma na jinsi mnavyoitumia Siasa ktk Maandamano kama kigezo halafu mnafanya Uhalifu.

    Acheni upumbavu wenu Mtii amri bila shuruti kama raia wema ama sivyo mtamezwa na Mamba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...