Mkurugenzi Mkuu wa Helvetic Solar Contractors Eng. Patrick Ngowi akiwa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alipofika katika ofisi hizo mapema leo kwa ajili ya mazungumzo na kuhojiwa katika kipindi cha Business Edition, kitakachorushwa Ijumaa hii saa 2 na dakika 15 usiku, Capital TV.
Dar es Salaam. 21 Mei, 2013. Mkurugenzi Mkuu wa Helvetic Solar Contractors Eng. Patrick Ngowi ameendelea kutoa rai kwa vijana nchini Tanzania kuwa na moyo na bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao za maendeleo na kujikwamua kiuchumi.
Eng. Ngowi ambaye pia ni mshindi wa ‘Forbes 2013: 30 under 30: Africa’s Best Young Entrepreneurs’ alisema maneno hayo mapema leo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alipofika kufanya ziara na mahojiano maalum katika kituo hicho.
“Vijana wa kitanzania wanafursa nyingi sana katika nchi yetu, imefika wakati sasa vijana wajitambue kwamba wanaweza kutimiza ndoto zao kadiri bidii zao zitakavyowatuma. Kwa mfano, mi nilianza na mtaji wa shilingi milioni mbili, lakini hivi sasa nilipofikia biashara yangu imekua na nimeweza kufanya maajabu makubwa katika soko ukizungumzia swala ya nishati ya jua,” alisema Eng. Ngowi.
Aliongeza, “Kinachotakiwa ni kuwa mbunifu katika biashara unayofanya, kuwa na ujasiri pamoja na umakini wa kile unachokipenda na pale unapotaka kufika. Yote yanawezekana na kijana yeyote anaweza fanikiwa.”
Pamoja na hayo Eng. Ngowi aliwapongeza sana IPP media kwa mafanikio yao waliyopata katika kipindi chote tangu kianzishwe, ikiwemo tuzo ya ‘Number 1 Super Brand’ katika Afrika Mashariki hivi karibuni.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alimpongeza kwa mafanikio yake na kumshukuru sana Eng. Ngowi kwa ugeni wake.
Picha na habari na Amani Nkurlu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...