Lady Jay Dee

Na Mwandishi Wetu
IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Mwandishi wa habari hii alimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kama nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa.
Mhe Makala
"Na siyo Waziri Makalla tu, pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshatoa fuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
"Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka...."  anasema Ruge.
Kushoto ni Dkt Emmanuel Nchimbi, wakati huo akiwa Waziri wa  Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo akiwa na Mhe Joseph Mbilinyi '"Sugu" na Ruge Mutahaba baada ya kuwapatanisha
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliibuka hadharani kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na blog yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumla, tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2013

    What an utter nonesense,one would think ministers and their deputies have better things to do-FACT.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2013

    Waziri ana mambo mengi ya kufanya ebu malizen matatizo yenu wenyeww

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2013

    Ruge ana matatizo makubwa. Anatumia vibaya vyombo vya habari. Hivi huoni aibu kuwa na ugomvi, mara Mr. Sugu, mara Lady Jaydee na Diamond. Samahani nahisi una wivu uliopitiliza. Hupendi maendeleo ya wenzako! Unapenda wanamziki wasio jituma. Angalia Mr. Sugu alikuwa musician na politician nawe hukupatana naye. Lady Jaydee, musician plus mjasiriamali mkubwa, pia umeanza mzozo nae. Acha hizo kabisa, tumia radio station kuleta maendeleo na si kupiga vita maendelo. Naungana na mdau wa hapo juu, kweli waziri kufanya kazi ya kumpatanisha Ruge na Jay dee ni kujisusha sana. Namshauri Mr, Ruge ili jambo hili lisijirudie tena ajisalimishe kwa Aunt Sadaka. You need Pschycological counselling. Utapatanishwa na wangapi na utarudia ugomvi na mastaa wangapi? Mwone Aunt sadaka before it is too late.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2013

    mbona kuna matatizo mengi ktk nchi hii? kwa nini tushughulikie watu wenye bifu?? kha! basi tuangalie mabifu yote ikiwemo ya waume na wake zao, wasichana na ma boyfriend wao... mabifu ya mabosi na wafanyakazi wao! kama kuna tatizo si kuna mahakama? kama kuna mtu katenda uhalifu watashitakiana watalipana wewe waziri una jukumu gani hapo? nadhani tujaribu ku clear mafaili yaliyojaa kwenye meza zetu... au better still muanze hata kuhudhuria mazishi ya wana michezo wote!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2013

    Mnhhh !

    Tunawekeza katika Mifarakano na sio Biashara.

    Kazi ipo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2013

    Mdau wa 3 juu.

    Afisa anapokuwa katika Senior Mangement level yaani(Mtendaji Mwandamizi), KTK MANAGEMENT ANATAKIWA KUWA KAMA BONDIA!

    ''IN MEETING MANAGEMENT STRATEGIES THE EXECUTIVE WEARS GLOVES AND BOX DOWN OTHERS''

    INA MAANA NDG. R.MUTAHABA ANATAKIWA APIGANIE MAJUKUMU YA NGAZI YA MADARAKA ALIYONAYO KWA MASLAHI YA TAASISI YAKE AKIWA KAMA BONDIA!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2013

    Hivi kwa nini kila ugomvi wa ruge serikali inaingilia?mbona ugomvi wa wasanii na madj hakuna hata mjumbe wa kata anayezungumzia?who is ruge katika nchi ya watu 45M au tunataka kuitumia radio yake kisiasa?

    ReplyDelete
  8. kuwapatanisha ruge na jide ni kupoteza muda. nampongeza jide aka komando kwa kumpa jamaa live. ruge acha wivu! common

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2013

    Pinki Jaydee una matatizo wewe sasa kunani hupikei simu wakati mashambulizi umeyaanzisha mwenyewe mwenzio yuko tayari kuwekwa kitimoto. Biashara imekushinda punki Jaydee ama ni nini. Acha kulialia kama mtoto wa kambo komaa na fanya biashara kama haiendi nenda kaajiliwe na vikundi vya taarabu na ngoma. Na wewe Ruge fanya kazi bila bifu mihela yote hiyoo bado una mnyanyasa pinki? Kwa nini hutangazi matukio ya hoteli ama mgahawa wa pinki? Kwani ni bure halafu hutaki hata kupiga miziki ya pinki tabia gani hiyo wewe Rugemalira? Kuwa kidume acha kugombana na mademu bwana inatutia aibu sisi wanaume. Gombana na sugu siyo mademu bwana. Ok michuzi post huo wosia wangu

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 11, 2013

    huyu Ruge ana matatizo sana nadhani hii yote ni jeuri na kiburi cha pesa huwezi kugombana na kila mtu, kama alivyoongea aliyetangulia hapendi maendeleo ya watu wanaotaka kujikwamua kwa ujasiliamali badilika .

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 11, 2013

    Mdau uliomjibu mdau number 3 ina maana unakubaliana na Ruge kugombana kila wakati na wasanii wanaoinukia na kufanikiwa..mdau number tatu amesema kweli..na kuhusu Waziri kukaa na kuwapatanisha ameamua kiubinadamu sio kwamba hakuna majukunu yapo ila ameguswa na hili hivyo mwacheni afanye alivyoona.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 11, 2013

    Kwa ufupi JD kwishne!
    Huwezi kushindana na Ruge 'mjini sku nyingi'

    Kama umesha haribu hella na sasa Benki wanataka cha kwao, inabidi tu uwe mpole ila, mjini bila ya huyo mshkaji..inakua ngumu au urudi kwenye Gospol!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 11, 2013

    Ngoja nipite zangu miye maana gogoro la wakubwa cmchezo,"mambo ya Ngoswe tumwachie Ngoswe mwenyewe..."

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 11, 2013

    Hayo ni maswala binafsi ya kibiashara. Waende mahakamani sio kutupigia kelele. Kuna kesi nyingi za kibiashara mahakamani, kwa mfano TBL na Serengeti Breweries wana kesi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 12, 2013

    We Anon unayesema Jide kwishney na mjini bila Ruge muziki hauezekani una fikra mgando.
    Ndo nyie watu wenye LOW SELFE ESTEEM,hebu nenda kwa wataalamu ukasaidiwe kwanza ndio nyie mkiambiwa hiki hakiwezekani mnarudisha mikono nyuma.
    Hivi unadhani watu wasipokua na uthubutu wa kusema HAPANA au IMETOSHA itakuaje?Unahisi ni wangapi wameshachezewa rafu na wamekaa kimya?Unahisi maamuzi ya JD yatawafungua wangapi toka kifungoni?Anaweza asiwe na approach nzuri lakini she may be right too, Inategemea analikabili vipi tatizo
    Watanzania tuache uoga WAKEUP!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2013

    Mdau anayesema Ruge inabidi awe kama bondia ndio uongozi mzuri! Hizo ni pumba tu! Ungana na Ruge mpate ushauri kwa Aunt Sadaka na wengine wote wanaotetea huo upuuzi.Mimi simjui Lady wala Ruge, ila kwa maelezo na taaluma yangu ya Udaktari naomba Ruge na hao wanotetea mjisalimishe kwa Aunt sadaka for(Psychosocial Support. Ruge anataka akikusaidia uendelee kuwa chini ya utawala wake milele. Badala ya kufurahia maendeleo ya wale aliowatoa chini na kuwakuza kimusic anataka wao waendelee kumwabudu. Hilo ni tatizo kubwa kisaikolojia. Ona mfano mzuri wa Mr. Masama au Madam Ritha, wanafurahi kuona wale waliowasaidia wanafanya vizuri. Ruge anaumia na kumpiga vita yule aliyemsaidia na kupanda juu. Kaka sikia ushauri wangu hilo ni tatizo kubwa lishughulikie!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 23, 2013

    Ninamuunga mkono JD kwa ujasiri kama mama na kama mwanamke, kusema ukweli daima na uongo ama kujikomba ni MWIKO. Wanamuziki wangapi wanajikombakomba kwa hao ma freemason..., kwani hatuwajui?? N nyie Serikali mbona mambo ya msingi hamyatolei maamuzi kazi kukimbilia kazizi zisizo na tija kwa Watanzania??? JIDE, UKOMBOZI WA MTU NI KUANZIA NA FIKRA NA KUJITAMBUA, MIMI NAKUUNGA MKONO, KUJIKOMBA HAKUFAI NI UTUMWA. NI BORA UPATE KIPATO KIDOGO CHENYE HESHIMA!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 14, 2013

    ur right mdau, ruge kazidi kuwakandamiza wanamuziki wanaopitia kwake

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 11, 2013

    Comando

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...