MZEE JAMES GERALD
MANDAWA WA KIWALANI,
DAR ES SALAAM,
Inapenda kutoa shukurani za dhati
kwenu wote mlioshiriki kwa moyo wa upendo katika kufanikisha shughuli za msiba
wa Mzee wetu Mpendwa James Gerald Mandawa.
Tunawashukuru sana
kwa faraja na ushirikiano mkubwa mliotupatia katika kipindi hiki kigumu sana cha kuondokewa na
Baba yetu Mpenzi, ambaye tulimpumzisha katika nyumba yake ya milele huko
shambani kwake Kiluvya , DSM.
Shukurani ziwafikie Madaktari na
wauguzi wa hospitali ya Hindu Mandal, DSM na hasa Dkt R. Kaushik , Menejimenti
na wafanyakazi wa TASAF Makao Makuu,Uongozi na wafanyakazi wa PRIDE –Arusha,
Uongozi na wafanyakazi wa DAWASCO Ilala Uongozi, wana jumuia na kwaya ya kanisa la
Kianglikana, Mt. Thomas –Yombo, majirani na marafiki wote.
Ni vigumu kuwataja wote, lakini
tunawaomba wote mpokee shukurani hizi kwa moyo mkunjufu.
“Baba,
tulikupenda sana , kuondoka kwako
kumekuwa ghafla sana , lakini
tunamshukuru Mungu kwa yote”.
Familia inapenda kuwataarifu na
kuwaomba mshiriki pamoja nasi kwenye
mkesha wa kumaliza msiba, tarehe 24 kuamkia 25 Mei, 2013- Kiwalani, na kwenye
misa ya shukurani itakayofanyika siku ya jumamosi tarehe 25 Mei, 2013 saa mbili
asubuhi, kwenye kanisa la Mt. Thomas, Yombo-Kiwalani, DSM.
BWANA ALITOA, BWANA
AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMEN.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...