Habari na Picha na 
Ramadhan K. Namkoveka
Timu ya Tanzania ya kuogelea imerudi jjumatatu saa 1.30 usiku ikitokea Lusaka, Zambia, baada ya kushiriki mashindano ya CANA kanda ya tatu na nne yaliyoshirikisha nchi 10 za Afrika mashariki, kati na kusini. Mashindano hayo yalifanyika kuanzia tarehe 25 hadi April 28 katika maeneo ya kituo cha maendeleo ya olimpiki. 
Timu ya Tanzania ilikuwa na wachezaji 18, hata hivyo haikuweza kupata medali tofauti na ilivyotarajiwa. Hata hivyo waliiweza kuimarisha muda wao ambayo inaonyesha kwa kuogelea Tanzania inakuwa siku hadi siku. 
Sonia Tumiotto alitokeza wa nne kwa kutumia muda wa 3.17.75 katika mtindo wa Breaststroke. Shamrad Magesvaran kwenye mita 50 backstroke aliweza kutumia muda wa sekunde 36.13 ambapo mshindi alikuwa ni Luan Grobbelaar kutoka Afrika Kusini. 
Muda wa kufuzu mashindano ya dunia yatakayofanyika Barcelona mwezi Julai mwaka huu ni sekunde 23.11 kwa muda B ambapo Hilal alitumia sekunde 25.36. Hii inaonyesha kuwa karibuni tu mchezo utatoa matunda mazuri.
 Licha ya kuwa mashindano yalikuwa ni magumu lakini tulifarijika wakati balozi wa Tanzania nchini Zambia mheshimiwa Grace Joan Mujuma alipoweza kuhudhuria mashindano hayo ya siku nne jukwaani pamoja na viongozi waliombatana na timu hiyo ikiongozwa na Ramadjhan Namkoveka na pia baada ya mashindano aliialika timu imtembelee ofisini kwake. 
 Hilal Hilal akiruka ktk 100 freestyle

 Shamrad Magesvaran akiogelea 200 freestyle
 Sonia Tumiotto akiogelea mita 400 freestyle
 Balozi Grace Mujuma (tshet nyekundu) akiwa na timu ya Tanzania katika  mashindano ya kuogelea jijini Lusaka
 Balozi Grace Mujuma(kushoto) akiwa jukwaani akiangangalia mashindano ya kuogelea
Tanzania ya kuogelea imerudi jijini Dar es salaam ikitokea Lusaka,
Viongozi wa timu ya kuogelea Tantzania walipoenda kumsalimia ofisin kwake Balozi wa Tanzania nchini Zambia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...