Msanii
wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani
wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao
Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri
jioni ya leo wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua
msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na
kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.
Aidha msimu huo umekwenda
sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA,ambapo
msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa
hizo kwa umoja wa maendeleo,huku neno TWENZETU likitumika kama neno
rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati
rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi
mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia
wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na
kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.
Msanii mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya leo.alipowaangushia maneno kadhaa na umati kulipukw ana mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao mpya.
Maelfu ya Watu wakiwa ndani ya uwanja wa jamuhuri jioni ya leo wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM kilipokuwa kikizindua msimu wake mpya.
Pichani shoto ni Mkurugenzi wa vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri jioni ya leo,wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea,Nape alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha maelfu ya watu.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.
"Muziki wa kizazi kipya, aka bongofleva katika miondoko ya Hip Hop."Hapa umesema kitu kimoja.
ReplyDeleteBongofleva is Tanzania's own version of Hip H0p ambao ndio huo muziki wa kizazi kipya.
In short, Bongo Flava is Hip Hop, Tanzania style!!
Bongo kumekucha! Yaani umati wote huo umeamua kwenda kuburudika baada ya kazi za wiki nzima.
ReplyDelete