Kaimu mganga mkuu wa serikali Dkt. Mohamed Mohamed akifungua mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala leo jijini Dar es salaam waliokutana kujadili mafanikio, changamoto na mipango mbalimbali waliyonayo katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba za Asili na Tiba Mbadala wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Paulo Mohammed akitoa ufafanuzi wa hali halisi ya Tiba za Asili na Tiba mbadala nchini Tanzania na mpango wa serikali wa kuendelea kuthamini huduma inayotolewa na wataalam hao wakati wa mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala.
Mratibu wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Rose Shija akisoma salam za mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatora leo jijini Dar es salaam ambaye amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kutatua changamoto zinazowakabili wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala.
Mtafiti mwandamizi mkuu wa Idara ya Utafiti wa Tiba Asili kutoka Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu Hamis Masanja Malebo akitoa mada kuhusu historia ya Tiba za Asili na uhusiano uliopo katika matumizi ya mimea ya asili kati ya tiba za asili na tiba mbadala na tiba za kisasa katika utengenezaji wa dawa. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Sehemu ya wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala waliohudhuria mkutano wa Baraza la Wataalam wa tiba hiyo wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...