Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua akizindua mpango wa maktaba ya dijitali kwenye shule ya msingi ya Nganana wilayani Arumeru May 10,2013. Wengine pichani kutyoka kushoto ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinoloji, Profesa Makame Mbarawa, Mbunge wa Rungwe Magharibi, Profesa David Mwakyusa, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia cha Mandela, Bulton Mwamila na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Nganana , Samweli Paanjo.
Wanafunzi wa Shule ya Misingi ya NGanana wilayani Arumeru wakionyesha kifaa cha elektrononiki kiitwa Electroni Reader che uwezo wa kuhifadhi vitabu zaidi ya 2000 kila kimoja katika uzinduzi wa Maktaba ya Elektroniki uliofnywa na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda kwenye shule ya Misngi ya Nganana., May 10, 2013.
Baadhi ya washiriki wa sherehe za uzinduziwa maktaba ya elektroniki kwa shule za msingi uliofanyika kwenye shule ya Msingi ya Nganana May 10, 2013. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo pinda.(Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2013

    Kidijtali!

    Watoto watakuwepo Kidijitali zaidi mwanawane.

    Tunahitaji tuitumie nafasi hiyo Muhimu kuwaingizia vitu muhimu na vyenye tija kama :

    1.Mitaala ya Masomo,
    2.Mafunzo na malezi ya tabia njema,
    3.Michezo inayokuza uelewa zaidi,
    4.Ujenzi wa uwezo binafsi,
    (Capacity building)
    5.Uwezo wa kufikiri na ufahamu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2013

    Kwanza nashauri vitu hivi vya electronic vinatakiwa vitengenezwa na sisi wenyewe na siyo kuwa soko la nchi zingine, pili kama alivyosema mwenzangu hapojuu tuwajengee watoto uwezo wa kufikiri na ufahamu, kwa kutumia vitu kama hivyo tunaua uwezo huo ndo tunajivunia nini sasa.
    Kwa maneno mengine tunatakiwa tuwafundishe watoto hawa namna ya kutengeneza hizo "candles" na siyo kutumia tu hapana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2013

    Anyway nivizuri,it's all about Technology. Ila bado inasikitisha Kwamba ndani ya Tanzania hii hii, vijijini ndani huko bado kuna wanafunzi wa shule za msingi wasomea chini ya miti, shule zilizojengwa Kwa udongo na kuezekwa Kwa makuti, wanakaa chini hawana dawati. All these advantages go to those in towns. what a country?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...