Kaka michuzi habari za leo.

Kutokana na mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha hapa Dar es salaam, sehemu hii ya barabara ya Mwepu kando kabisa ya jengo la Wizara ya Katiba na Sheria imeharibika kwa kutitia na kutengeneza shimo ambalo sio tu linahatarisha maisha ya watumiaji wa barabara hiyo lakini linaleta usumbufu na foleni kubwa. Ni takribani wiki zaid ya mbili sasa lakini wahusika hawajachukua hatua yoyote. Tunaomba wahusika wachukue hatua ili kulinda usalama wa watumiaji wa barabara hiyo muhimu.

Zifuatazo ni picha zinazojieleza zenyewe kusaidia wahusika kuona hali halisi.

Shukrani kaka



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2013

    Haya mashimo yanatisha sana. Siku moja baada ya mvua na kujaa maji, nilitumbukia kwenye shimo moja na kukwama.Tena ilikuwa ni karibu na hospitali ya magonjwa ya akili.Basi nikajikuta nimezungukwa na wahuni kama sita hivi,wote chini ya miaka sita au saba hivi.Gang leader akaniuliza,hilo gari umeazima nini, na una wazimu, hukuliona hilo shimo? I was having a bad day but he cheered me up.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2013

    Wabunge mlio wachagua wapo Bungeni wanatukana matusi makali na kutaka kuraruana mashati wakati kwenye majimbo yao kuna barabara zimeoza na mashimo ya kutisha!!! hao ndo wabunge mlio wapigia kura.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Si munaona wazi,hapo niair port ya mwanga toka kwa watani wa jadi, ajaribu kuzuia ziara ya mkuu wa kule nanihii. Ngija tuone kama ataweza. kwi kwi kwi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...