Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu Mkoa wa Kigoma Mwl.Joseph Mwangamila,wa pili toka kushoto akikabidhiwa msaada wa Kompyuta Tano zenye thamani ya shilingi Milioni 6 na mshindi wa”Vodacom Mahela”Bw.Valerian Kamugisha ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho kwa niaba ya Vodacom Foundation.Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon na Mwenyekiti wa bodi wa Chuo hicho Askofu Dkt Gerald Mpango watatu toka kushoto.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu Mkoa wa Kigoma Mwl.Joseph Mwangamila pamoja na Mwenyekiti wa bodi wa Chuo hicho Askofu Dkt Gerald Mpango wakiwa na nyuso za furaha wakiinua moja ya Kompyuta juu kati ya tano zenye thamani ya shilingi Milioni sita,walizopewa msaada na mshindi wa ”Vodacom Mahela”Bw.Valerian Kamugisha(kulia) ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho kwa niaba ya Vodacom Foundation.anaeshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu Mkoa wa Kigoma Mwl.Joseph Mwangamila(kulia)akimkabidhi sehemu ya msaada wa Kompyuta Tano zenye thamani ya shilingi Milioni 6,Mwanafunzi wa chuo hicho,Rehema Romani,baada ya kukabidhiwa na mshindi wa”Vodacom Mahela”Bw.Valerian Kamugisha,wa pili toka kushoto,kwa niaba ya Vodacom Foundation.Anayeshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation, Bi.Grace Lyon.
Picha ya pamoja.
Ama kweli nanianasema sio tamu Fedha?
ReplyDeleteSuti imetulia tofauti na alivyokuwa hapo kabla wakati akienda chukua 'mzigo' wake 100Mil. akiwa katika mashati ya kawaida.
Bwana Mapesa Vodacom Mahela Valerian Kamugisha anazidi kung'ara!!!
Maisha bwana, MUNGU akiamua basi!
ReplyDeleteKijana ndio hivyo tenaaaaa!
kwa hiyo sasa zimebakia milioni 94. Mungu amusaidie kijana kwani ana roho nzuri.
ReplyDeleteila aangalie asitoe misaada mingi halafu akaishiwa
Mdau wa 3
ReplyDelete.......
kwa hiyo sasa zimebakia milioni 94. Mungu amusaidie kijana kwani ana roho nzuri.
ila aangalie asitoe misaada mingi halafu akaishiwa
.......
Usiwe na wasiwasi MUNGU NI TAJIRI SAAANA Ndugu V.Kamugisha kamwe hawezi kuishiwa tayari amesha chaguliwa na Mwenyezi, kwa kuwa akitoa sana ndio atapata nyingine zaidi!
Kwa kweli SIR GOD hama Mshirika!
ReplyDeleteNchini Tanzania tupo takribani 45Mil. miongoni mwetu wengi walipenda wazipate Tsh. 100.Mil lakini SIR GOD akamchagua ndugu Valerian Kamugisha !!!
Wadau ni kama anavyosema Madu wa 5 hapo juu,
ReplyDeleteRiziki haina kigezo cha kuwa na ujanja wala haraka ya kuwa mjanja sana ndio utafanikiwa ama kuwa na haraka sana na kutumia nguvu nyingi ndio vigezo vya mafanikio la hasha!
Ni kama ndugu yetu Kamugisha hakuwa na haraka wala hakutumia Mabavu kuzikamata Tsh. 100Mil. ila ni kutokana na uwezo wa MWENYEZI ASIYEKUWA NA FITINA WALA MAJUNGU!!!