Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma  Deusdedit Nsimeki akipanga maneno ya tembo kulingana na uneno /uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

-------------------------------------------------- 

JESHI  la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya Tembo  18 yenye uzito wa kilo 84 yenye  thamani ya Tsh216,000,000/ambapo meno hayo 18 ni sawa na dola 15 elfu za kimarekani pia ni sawa na Tembo tisa waliouwawa .
 
 Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma  Deusdedit Nsimeki amesema kuwa tukio hilo la kukamata meno hayo lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku  katika kijiji cha Majala kata ya Nandembo iliyopo wilaya  ya Tunduru mkoani Ruvuma .
  
 Kamanda Nsimeki amesema kuwa  tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo lilitokea  baada ya askari polisi wa wilaya hiyo kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa hao lakini bahati mbaya watuhumiwa hao walikurupuka na kuacha mizigo ya meno hayo iliyokuwa imefungwa kwenye mifuko tofauti tofauti.
   
 Alisema kuwa watuhumiwa waliokurupuka walikuwa wanne huku kila mmoja na baiskeli ambazo walikuwa wamebebea meno hayo na kwa upande wa watuhumiwa wa meno ya tembo kukurupuka bila kutiwa mbaroni na jeshi hilo limekuwa ni tukio la pili la kwanza  lilitokea katika kijiji  cha Hanga wilayani Namtumbo na la pili ndiyo hilo la wilaya ya Tunduru zote za mkoani Ruvuma .
  
 Aidha kamanda alisema kuwa jeshi la polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao wamejificha na wanajihusha na matukio hayo ya ujangili kwa wanyama  na hasa tembo.
             
Pia ametoa wito kwa wananchi uendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo vya uhalifu wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi na wananchi.

Picha na habari kwa hisani ya Demashonews.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2013

    Nionavyo mimi hawa majambazi wataendelea kuua hawa tembo maadam kuna faida kuu katika biashara hiyo.Mnyama mkubwa kama nyumba auliwa kwa meno mawili tu. Aibu na ni ukatili mkuu. Nchi inaweza kuharamisha biashara hiyo ikipitisha sharia ya ukatili:(unreasonable laws)
    Ukikamatwa na kilo moja ya pembe,utasota miaka ishirini jela, ukikamatwa na kilo zaidi ya moja, kamba shingoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...