Na Ripota wetu Washington
Kijana Edward J. Snowden (pichani), mfanyakazi wa zamani wa wakala wa Usalama wa Taifa  wa Marekani (NSA) aliyevujisha nyaraka nyeti zinazohusu mawasiliano ya watu yanayonaswa na wakala hiyo kwa vyombo vya habari amefunguliwa mashitaka ya kuvunja sheria ya Ujasusi na kuiba mali ya serikali ili kuvujisha taarifa nyeti kwa gazeti la Guardian na Washington Post, Idara ya Sheria ya nchi hiyo imesema.
Kila kosa katika hayo matatu aliyoshtakiwa nayo yanabeba adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, na habari zinasema huenda akaongezewa mashtaka. Zaidi ya shitaka la wizi, mashtaka mengine mawili ni kufanya mawasiliano yanayohusu taarifa za ulinzi wa taifa, na kuwasilisha kwa hiari yake taarifa nyeti za kiintelijensia kwa mtu asiye na idhini kuzipata.

Mashtaka hayo yalifunguliwa Juni 14, 2013 na waendesha mashtaka wa wilaya ya Mashariki ya Virginia, ambako ndiko kesi nyingi za usalama wa Taifa za Marekani huendeshwa. Maafisa wa Marekani wamesema tayari wamewaomba maafisa wa Hong Kong, ambako Snowden anaaminika amejichimbia, kumtia mbaroni  wakati maombi ya kumpeleka Marekani yakiandaliwa.
Jaribio la kumhamishia Snowden nchini  Marekani huenda likasababisha zogo refu la kisheria ambapo matokeo yake hayajulikani. Makubaliano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Hong Kong yanahusisha pia kipengele cha kutomhamisha mtuhumiwa yeyote wa kisiasa toka nchi moja hadi ingine, ambapo Snowden anaweza kudai kuwa kesi yake ni ya kisiasa.
Maswala yote ya Hong Kong yanayohusu usalama wa Taifa hushughulikiwa na Serikali ya China huko Beijing. Katibu wa zamani wa Usalama wa Hong Kong Bi Ip ambaye sasa ni mbunge amesema leo kuwa hakuna jinsi bali kukubaliana na Marekani na hati ya kukamatwa Snowden ikija polisi wao watamsaka na kumtia mbaroni.

Hata hivyo, Bi Ip amesema kwamba Snowden anaweza uhamisho wake kwa kudai alichokitenda ni kosa la kisiasa, ama anaweza kuomba hifadhi ya ukimbizi, na kwamba kesi aina hiyo huchukua hata miaka 10 kukamilika.
Juma lililopita mamia ya watu waliandamana kwenye mvua nje ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Hong Kong wakiwataka maafisa wao wasitoe ushirikiano kwa ombi lolote la kumhamisha Snowden.

Mashtaka kama anayokabiliwa nayo Snowden ni ya saba chini ya utawala wa Rais Obama, wakati utawala wa marais wote waliopita  ni mashtaka matatu tu yaliyofunguliwa dhidi ya ofisa wa serikalikuvujisha taarifa nyeti kwa vyombo vya habari.
Snowden, ambaye Ijumaa iliyopita alitimiza umri wa miaka 30, alikimbilia Hong Kong mwezi uliopita, baada ya kuacha kazi yake ya kijasusi katika kituo cha Hawaii. Ameshavujisha taarifa kibao nyeti sana kwa gazeti la The Guardian, ambalo limekuwa likichapisha mfululizo wa makala kuhusu serikali za Marekani na Uingereza kusikiliza mawasiliano ya watu kwenye mitandao na simu.
Kwa kuvujisha taarifa hizo nyeti, Snowden amefungua dirisha lisilotarajiwa kuhusu mwenendo wa kiintelijensia wa N.S.A, ikiwa ni pamoja na kukusanya kwake kwa taarifa karibu zote za simu zinazopigwa Marekani pamoja na mkusanyiko wa email za kutoka watu wan je ya nchi hiyo kutioka katika makampuni makubwa ya mtandao, ikiwa ni pamoja na Google, Yahoo, Microsoft, Apple na Skype.
Snowden, ambaye alisema alishangazwa kwa kile alichoamini kuwa ni hatua ya NSA inayoingilia mambo binafsi ya Wamarekani na watu wan je ya nchi hiyo, aliliambia gazeti la The Guardian kwamba amevujisha nyaraka hizo nyeti kwa kuwa anaamini mipaka ya kufuatilia habari za watu iamuliwe sio na maafisa wa serikali bali rais wa Marekani.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2013

    Mambo kama hayo yanaweza tokea hata huku kwetu. Hivyo idara za usalama inabidi kujifunza na kutobadilisha mifumo ya kuwapata vijana waadilifu na wazalendo wa kweli kufanya kazi nao.
    Sasa kijana hakuweza maliza masomo yake, pia hata kwenye mafunzo ya kijeshi hakuweza kufuzu vizuri yote hayo ni viashilia vya kuwa na mashaka. Hila jamaa wakakomaa nae wakampatia kazi.

    Soma kwa idara zetu pia, vetting izingatiwe sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2013

    Mzuri Huyo natamani awe mume wangu .

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2013

    Who care!

    ReplyDelete
  4. i agree with snowden bcoz of free speech and that of unright of communications freedom.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...