Marehemu Jaji Khamisi (Kashi)

Msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee masinde,samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi Amefariki dunia mchana wa leo katika hosptali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.

akizungumza na Ripota wetu raisi wa shirikisho la wasanii Nchini,Bw. Mwakifwamba amesema kuwa tasnia yake bado inaendelea kukumbwa na majanga  lakini amedai yote ni kazi ya mungu.

Nae mzee masinde ambaye alikuwa nae katika kundi moja akiwa kama kiongozi wake amesema kashi ni msanii ambaye alikuwa mpiganaji na kwa hakika ni pigo kubwa katika tasnia yetu
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi)
mahali pema pepponi Amini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2013

    Yumkini alikuwa mwenye mwisho mwema.

    Sote ni wa Mungu na kwake tutarejea.

    Pole kwa kila muhusika.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2013

    hapo juu, maneno mazuri sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...