Ankal pole sana na machofu ya safari.
 Nilikuwa naomba niwaulize wadau wa Globu yetu swali kidogo maana sina uhakika nifanyeje. 
Mfano mtu anataka kurudi na kufanya shughuli zake Tanzania kutoka ughaibuni akiwa na familia yake,  ni Kata gani katika mkoa upinna wilaya ipi unaweza kumshauri aje kuishi na kwa nini na ni Kata gani itamfaa yeye kuendesha biashara zake na kwa nini. 
Vigezo vya kuzingatia ni pamoja na miundo mbinu (maji, umeme, barabara, usafiri n.k), usalama, huduma muhimu (shule, hospitali etc), vivutio vya kuwekeza, gharama za kodi n.k

Natanguliza shukurani.

Mdau Majuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    We unaonekana muoga?! Kwani hauna ndugu wa kuwauliza au kwanini we mwenyewe usiende kuchungulia na kufanya upembuzi yakinifu then uta decide. Usije ukajiroga mwana ukabeba familia yako ukaingia bongo kurupu mwana utalia!!! Michuzi hawezi kukwambia unampa mtihani wa bureeee!. Michuzi mwenzio anakaa TANDIKA sasa we TANDIKA utapaweza? Alafu inavyoonekana hauna hata kibanda japo cha vyumba viwili sasa sijui unataka kwenda kufanya nini bongo? Bongo sio SINGAPORE kaka shauriyako!JENGA KWANZA NDIO UFIKIRIE KURUDI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    manzese ni pazuri sana. Barabara na maji yako.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    Ndugu uliye ughaibuni,nakushauri usirudi kichwa kichwa na familia yako,kwa njoo ujionee mwenyewe,hakuna
    kata au tarafa yeyote iliyo wazi kila
    kona ardhi wameuziwa wawekezaji,
    na bado nchi inaendelea kupigwa mnada
    kwa hivyo usitegemee kabisa kuwa unakuja kwenu . labda ununue hisa kigamboni ambako nako kumeuzwa na mnada unaendelea kwa sehemu zilizo bakia

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2013

    we ungekutana na kingwendu alafu ungemuuliza hilo swali jibu lake lingekuwa we mwehu nini ebu jiangalie tena jiangalie kwa sana miswali ya hajabuhaju mwenzio siiwezi kuijibu we kalagabaho na majuu yako.

    ReplyDelete
  5. Rashid,usaJune 07, 2013

    Hakuna Hata sehemu moja,

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2013

    Inaonesha umakata miaka mingi huko nje ya nchi,mimi nakuambia huhitaji ushauri wowote ule, wewe nenda katembee ulikotoka na ulikozaliwa utajionea mwenyewe and than you will make your uwamuzi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2013

    biasahara ipi ya dhahabu, duka la rejereja, unga, au mifugo?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2013

    Endelea kuishi huko huko Mpaka midevu iote mvi usirudi! Umri ukishaenda sana na uwezo wa kuajiamulia mambo yako ukiisha na nguvu za kuweza kufanyakazi hakuna ndio uje! Utashangaa unatafuta nyumba ya kupanga marafiki zako wote ndio wababa wenye nyumba!!! Fanyia kazi ushauri huu Ndg yangu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2013

    Mdau wa majuu! swali lako ni zuri na pengine wengi wajiuliza hayo maswali.
    Kwanza kama huko hakieleweki yaani kama hutengenezi zaidi ya 50000usd kwa mwaka bora urudi.
    wapi urudi, nenda ukaexplore ujionee mwenyewe. inategemea una liasi gani na ni shughuli gani wataka kufanya. Usiogope kama hakieleweki bora kurudi mapema kabla hujadata.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2013

    Pole. kwani wewe ulizaliwa wapi?
    Kwa hivyo vigezo Nadhani ni bora ukabakia hukohuko.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2013

    Swali lako bado liko general sana. Ungeeleza ni shughuli gani mtu anayerejea nchini anatarajia kuwekeza ktk nini na kwa kiwango gani cha technology ili wanaomshauri wajue wapi panapomfaa. Tanzania ina fursa nyingi na kila sehemu ina fursa za kipekee ambazo pengine hazipatikani ama si nyingi katika maeneo mengine.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2013

    yaani watu wengine ni wavivu wa mawazo, nimekaa ughaibuni zaidi ya miaka 25 lakini nikitaka kurudi sitauliza watu mtandaoni, inavyoonekana mtoa hoja huwa HURUDI bongo kusalimia, kwa ungekuwa unarudi mara kwa mara majibu yote ungekuwa nayo, sas anza kwenda bongo kila mwaka na familia yako halafu tembelea sehemu mbali mbali, angalia wapi panakufaa wewe na familia yako, don`t bring this collective responsibility nonsense.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2013

    Ni kata, wilaya na mkoa uliyokuwa ukiishi kabla ya kwenda majuu!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2013

    Ushasema kurudi Tanzania. ukimaanisha ushaishi Tanzania sas ugumu uko wapi au unazuga. ungesema unataka kuja Tanzania ingekuwa ishu nyingine. Pamoja na hayo ukiwa huko natumaini ungekuwa na upeo wa juu kusoma vitabu na vipeperushi mtandaoni kujua hali halisi ya kitanzania. Au ndo hilo hujalijifunza sidhani linahitaji mtu kuingia darasani.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2013

    Pay consultancy to do for you that job.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2013

    My Friend sikupondi ila the way unavyouliza as if you are so special and of very high class. kwani inamaana you got no Idea about Tanznia!!! au wewe sio mtanzania au hujawahi kufika Tanzania au huna hata ndugu ambae huwa anakupigia story za Tanzania. you are asking as if ni Mtu kutoka Kazakstan anakuja kwa mara ya kwanza Tanzania kutafuta maisha. kama wewe ni Mtanzania na ni mzalendo na muungwana you should have answers kwa yote uliyoulizwa.
    best regards.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2013

    Njoo kwetu Mitaa ya Mihande Mgeni Nani Mbagala UZUNGUNI YA MBAGALA, Dar Es Salaa, utakula starehe kama upo huko huko Majuu!

    NATETEA HIJA YANGU KWA VIGEZO:

    1.MAJI:
    Hatuna Shirika kubwa linalogawa maji kama Dawasco isipokuwa tuna Wagawaji wa Maji wa uhakika wa Makampuni Binafsi, maji pressure ni 100% labda usipolipa Bili watakukatia.

    2.UMEME:
    Hauna shida haukatiki ovyo hataukikatika hayapiti masaa unarudi, na hata kama utakatika watu wengi wameweka standby zao za Solar Power juu ya mapaa ya nyumba zao kama huna Jirani yako utaongea naye atakuunganishia.

    3.USAFIRI:
    Hakuna shida kabisa ya usafiri kwa kupandia madirishani ktk mabasi, watu wanakaa level seat pia njia zinapitika kama unao usafiri wako ni uchaguzi wako kama upitie Kigamboni ama Mbagala Rangi 3 ambako kuna barabara nzuri sana na hakuna foleni.

    4.ULINZI:
    Polisi na Idara ya Usalama ktk Mbagala na Kijichi yote wanafanya kazi ya ziada sana, ni mara chache utasikia matukio na hata yakitokea Wazee wa kazi mara moja wanakuwa wamewajibika na wanakuwa wamewakamata wahusika.

    5.JAMII:
    Imeumbika kwa ustaarabu wa hali ya juu watu wa Dini tofauti wapo na kila mmoja na imani yake huku wakiishi kwa umoja amani na upendo, hutasikia Maandamano ama watu kushambuliana ktk Majukwa kwa misingi ya imani.

    6.BURUDANI:
    Kama ujuavyo ukanda wa Pwani ya kusini unashika kasi ya ajabu ktk medani za burudani karibuni Mahoteli mengi yako ktk Beach ya Kusini kuanzia Kigamboni hadi kuelekea Bongoyo na kwingineko hadi Visiwa vya Mbudya ktk Bahari ya Hindi, utakula starehe kama upo Key West Florida Marekani.

    Eneo letu lina pubs nyingi za kistaarsabu na majumba yamepeana nafasi hadi unapata hamu ya kumtembelea jirani yako baada ya utulivu wa muda Fulani.

    Sehemu za mapumziko ya mwisho wa wiki ni nyingi sana mfano FUN CITY, DAR ESALAAM ZOO, SOUTHERN BEACH ,DAR LIVE MBAGALA na zinginezo.

    7.UIMARISHAJI WA MAKAZI MAPYA:
    Mipango na miradi mingi ya makazi mapya ipo eneo letu mfano NSSF, NHC, MANJI na mingineo wamewekeza ktk makazi ya kisasa na huku kasi ya ajabu inaendelea.

    MBAGALA ILIYO CHEKWA NI ILE YA ZAMANI NA SIO YA SASA.

    KILA ANAYESIKIA AKITEMBELEA HUAMUA KUHAMIA HUKU AMA KUJENGA HUKU.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2013

    msaliti, mnyonyaji, kabaila, kaburu mkubwa weh!, kupe, mhujumu, beberu mkubwa weh...!
    huwezi kuikimbia nchi yako...halafu ukakimbilia nchi ambayo wananchi wake walijifunga mikanda wakaijenga kwa kujituma kufanya kazi kwa bidii...umeenda huko umewanyonya sasa unataka rejea huku ambako wazalendo wanaendelea kupambana kuijenga nchi yao...kiufupi baki huko huko hatukuhitaji huku...

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 07, 2013

    Ngudu masuala yako ni mazuri. Kwanza ujue kuwa TZ watu wana roho mbaya hususan kama unatoka au unakwenda majuu ikiwemo hata jamaa zako. Kabla hujafanya maamuzi ya kurudi TZ jiulize kama utaweza kurudi tena Ughaibuni. Pili kabla hujarudi TZ moja kwa moja jiulize kama una mtaji wa kuanzia $100,000/- na nyumba ya kuishi na gari. Kama unataka kuishi Dar, shughuli ni biashara za duka, salooni za nywele, kuosha magari, spea za magari, taxi, daladala, simu za mkononi, "used", nguo, viatu, nk. Mwanza, Arusha na Morogoro ni sawa na Dar kama utaishi kwenye makao makuu ya mikoa. Sehemu nyengine za TZ utaishi kwa kilimo na ufugaji wa kuku au ng'ombe. Zanzibar ni biashara ya Utalii lakini uwe tayari una "agents" huko ughaibuni. Kama una watoto wadogo hawana tatizo lakini kama unamatoto yameshafika miaka 12 na zaidi una mtihani. Njia nzuri ya kurudi ni uanze kwanza kuja taratibu wewe ukaanza kuweka maandalizi kwa kuanza kujenga nyumba pia kuleta mzigo wa vitu "used".

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 07, 2013

    KAMA UNAPIGA KIBUKU(CHIBUKU) NJOO UTAFURAHIA BONGO KAMA MIMI

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 07, 2013

    Nawashangaa mnao mrushia mitusi mdau mwenye swali. Ameuliza tu - ukiweza kumjibu sawa ukishindwa nyamaza. sa mitusi ya nini? kwlei ustaarabu gharama!
    Ushauri
    Naungana na aliyeshauri urudi pole pole - tembelea mikoa mbali mbali kwa mwaka kama mmoha hivi, sio lazima ulikozaliwa - wengine tulikozaliwa serikali imeiuzia wageni - angalia patakapo kufaa, jenga mahusiano na watu wa hapo - ukishapata taarifa zote, basi rudi huko uliko ujikusanye halafu unaandaa pa kuishi ukileta familia angalau wewe ndio unaowaongoza. Mkija wote wageni itakuwa kazi. Watoto wengine hata choo cha shimo hawajaona, wasije wakakaa kwenye vyoo vya uswahili bure!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 07, 2013

    MAISHA YA TANZANIA NI TOFAUTI KABISA NA YA MAJUU. nenda miezi yako sita kwanza ujionee kama unaweza. mwaka juzi mie nilienda nikakaa miezi 6, miezi miwili ya kwanza ilikuwa kama vile sikukuu kila siku, baada ya hapo real life ikaanza. ufisadi ni kila mahali. ila biashara nili-target high class so ilienda vizuri. umeme ulikatika mara chache so sikujali, maji nina simtank so siku-notice uhaba wake. watu ni wakarimu ila kila week kuna kutoa mchango wa arusi au sendoff au kitchen party u name it. beer zinanyweka kila siku but zinazoofisha afya. Ila kilichonishinda ni conveniences, ujambazi, wizi nk nikasepa zangu back to majuu nitarudi bongo kutembea tu

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 07, 2013

    Wadau wenzangu nawashukuru sana kwa majibu yenu. Mimi sipo ughaibuni ila nilikuwa nafanya utafiti mdogo tu kwa ajili ya mteja wangu (Kata moja hapa Dar) kuona jinsi watanzania mnauwelewa gani wa sehemu mnazokaa/ kufanya kazi na mnatoa mchango upi kwa maendeleo ya sehemu husika. Mteja wangu ana nia ya kubrand Kata husika (kama wafanywavyo nchi zilizoendelea, China na SA) ili kukaribisha uwekezaji wa ndani ili kuongeza ajira na pato la Manispaa. Kwakuwa biashara nyingi kubwa zinaondoka katikati ya Jiji na zile mpya huanzishwa nje ya CBD ni wakati muafaka kwa maeneo mengine kujinadi na kuvutia biashara hizo ili kuziongezea Manispaa pato kupitia kodi mbalimbali, ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, uwekezaji katika miundo mbinu, kupandisha gharama za ardhi (ikiendana na property tax), kuongeza usalama n.k. Majibu yenu yamenipa pa kuanzia.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 07, 2013

    rudi mkuu, njoo kata ya mafinga wilaya ya mufindi mkoani irnga kwanza hali ya hewa ni ya baridi kama ya majuu, usafiri na barabara ni nzuri kabisa, mawasiliano na mtandao upo vizuri, utalima chai na kunywa chai kwani wakati wowote ni wakati wa chai na piaa jamii inapenda wageni kama wewe

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 08, 2013

    watu wengine kwakuwavunja wenzie moyo hawajambo kama mtu hujuii nini chakujibu siukaa kimya kwani yeye hajui kama anandugu wa kumuuliza na kama ameona ndugu hawaeleweki kwa namna moja au nyingine eti aende akatembelee je kama aalijilipua kuja kuruni hakutamfaa acheni kuwakatisha watu tamaa mimi mwenyewe nasubiri wachangiaji wazuri wachangie mimi pia nina tatizo kama ya huyu muuliza swali

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 08, 2013

    Njoo Morogoro kuna kila kitu maisha ni mazuri saaana

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 08, 2013

    Njoo Morogoro kuna kila kitu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...