Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga (kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara pamoja na taasisi zake. Silima alitembelea taasisi zote za wizara zilizoshiriki maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akipimwa kilevi kwa kifaa maalum na Askari Polisi (kulia) wakati alipotembelea banda la Jeshi la Polisi katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakitoa vipeperushi vya wizara hiyo kwa wananchi na wanafunzi wa shule ya awali waliotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) akipewa taarifa za kazi mbalimbali zinazofanywa na Idara ya Uhamiaji na Afisa wa idara hiyo wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akimfundisha mwanafunzi wa shule ya awali jinsi ya kuzima moto wakati wa maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Julius Sang’udi (katikati) akimuonesha samani za ndani Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) wakati alipotembelea banda la Jeshi la Magereza katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Picha zote na Felix Mwagara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...