MBUNGE wa Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo, akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanambwewe waishio Dar es Salaam (MNDF), leo katika ukumbi wa Shule ya Msingi Ali Hassani Mwinyi, mjini Dar es Salaam. Wanachama hao walimwalika kwenye kikao chao cha kujadili jinsi ya kuuendesha mfuko huo kwa manufaa ya wananchi wengi.
 Katibu wa wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya wanamtandao wa Mbwewe waishio Dar  es Salaam, Hassani Msonde akizungumza mwanzoni mwa kikao
 Mwenyekiti wa Umoja huo, Rajabu Papa akifungua kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati ya Umoja huo, Fatuma Kikwappe akisoma risala huku viongozi wakimsikiliza kwa makini akiwemo Mbunge Bwanamdogo.
Kisha akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo
 Mbunge Saidi Mwanamdogo akiwakabidhi dola za Marekani, viongozi wa umoja huo, ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kufanikisha usajili.
 Mwenyekiti akimkabidi Mbunge Katiba ya Umoja. NA theNkoromo Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2013

    Je huu tunaonyesha mfano gani toka kwa viongozi wetu kutumia dola za marekani badala ya shillingi ya tanzania?

    ReplyDelete
  2. Dola kwa ajili ya nini? inamaana siku hizi wabunge wanatembea na dola badala ya Tshs?

    Ni hatari kweli kweli! Au kuwaonyesha hao Wanambwewe kuwa anazo? Shame to you Mwanamdogo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2013

    kwa kweli mheshimiwa ameboa sana,na hizo dola zake ambazo hata mia hazifiki,tunajua kwamba wanamiliki account za dola,lakini hajui yalipo maduka ya kubadili pesa?kikao cheyewe cha kawaida tu anapeleka hela za kigeni, tena kiduchu, mbona tunaona michango mikubwa watu wanatoa hela za madafu tena za kutosha.Ahamie kwa Mugabe wanakotumia dola kama anaona madafu yamechomsha.kweli hawa waheshimiwa wetu wana tofauti sana na sis tuliowapa 'kula'

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2013

    Wadau Mkubwa Mhe. mbunge ametumia DOLA ZA OBAMA ili aweze kufanya Usajili wa Dirisha Dogo ili aweze kutokea hapo kwa kutoa lawama kwa kuwa kama mnavyoona Dola zenyewe masifuri yake yapo chini ni 20 na za 50 mbili tatu hivi Kiasi cha kama hata Laki haifiki!!!

    Si mnajua tena?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2013

    Apew e Taarifa Prof. Ndulu Gavana wa Benki Kuu.

    Hili noi mojawapo la Kosa la Kibenki kwa kuwa ktk Moja ya ''CENTRAL BANK MONETARY POLICY INSTRUMENTS'' yaani Sera Kuu za Benki Kuu ni MORAL SUATION yaani KUWAPA MWAMKO WANANCHI hasa ktk Suala la kutumia Sarafu ya Ndani ya nchi ktk manunuzi na mzunguko wa matumizi ya kawaida wakiwa ndani ya nchi.

    Ina maana hata Mgeni akishaingia Tanzania anatakiwa abadili Fedha zake akiwa Uwanja wa Ndege ili aweze kufanya matumizi yake kwa Fedha za ndani akiwa nchini hadi siku akiondoka ndio alizobaki nazo atazibadili kuwa Dola akiwa Uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurudi kwao.

    Benki Kuu ilishatoa angaizo mara kadhaa ni vile Amri hizi hazitekelezwi, mfano nchini Rwanda ukiwa Mjini Kigali ukitumia Dola ama Fedha za Kigeni unakamatwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...