Baadhi ya wanawake wajasiriamali wadogowadogo wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini wakipatiwa elimu na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania hawapo pichani,kabla ya kupatiwa mikopo yao ya pesa isiyokuwa na riba ya zaidi ya shilingi Milioni 327 iliyotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI".mikopo hiyo inawawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini kujiendeleza katika biashara zao,na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.
Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane Bi. Rosena Rashid -Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akisaini kitabu cha orodha ya wakina mama wajasiriamali wadogowadogo waliokuwa wakipatiwa mikopo ya pesa isiyokuwa na riba ya zaidi ya shilingi Milioni 327 toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI"unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini, na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa.
Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane Bi.Rosena Rashid- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akipokea mkopo wa pesa kutoka kwa wakala wa M-PESA wa Vodacom Morogoro,Bw.Verus Bitahilo(alieketi)Kampuni hiyo inatoa mikopo kwa wanawake wadogowadogo wajasiriamali hapa nchini isiokuwa na riba wanawake hao walipokea mkopo huo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 327 kupitia mradi wake wa "MWEI" na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia wapili toka kulia walioketi ni Meneja wa mradi huo Bi.Grace Lyon.
Mwenyekiti wa kikundi cha Mother support Bi.Veronica Nyemele- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akionesha na kufurahia pesa zake alizopewa mkopo usio na riba toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI"unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini, wanawake 7500 walinufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni 327.
Sehemu ya wanawake wajasiriamali wadogowadogo walionufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni 327.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2013

    Hivi Morogoro kuna vijiji? Mbona kuzuri kama mjini,hizo nyumba mbona kama mjini wajameni,,Afande Sele na Stamina nakuaminieni na moro yenu.na pongezi kwa VODACOM kwa kuwafikia akina MAMA vijijini nchi nzima.tuna taka makampuni kama haya yanayo jali jamii.ni mm mdau wenu PAPINYO kutoka uingereza au UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...