Mkufunzi toka taasisi ya Risxcel, Sunny Ahonsi akitoa mada kuhusu Governance and Parliament kwa viongozi wa Bunge.Naibu Spika Job Ndugai (kwanza kushoto), Wenyeviti wa Bunge (Mhe Zungu na Mhe Mohamed Seif Khatib) wako Dubai katika mafunzo maalum kwao kama viongozi wa Bunge wakiongezewa uwezo katika maeneo ya Uongozi Bora, Uendeshaji wa Vikao na Mikutano na tathmini ya mifumo na uongozi wa kibunge duniani.Mafunzo hayo yanatolewa na jopo la wataalamu toka Uingereza kupitia taasisi ya Risxcel.
Mhe Job Ndugai akitoa maelezo kwa wenzake juu 'Leadership Values', Mafunzo hayo ambayo ni ya vitendo zaidi ni sehemu ya mipango ya Ofisi ya Bunge kuongeza ujuzi kwa wabunge na viongozi wake.
Mhe Zungu akichangia katika moja ya mijadala kwenye mafunzo hayo.
Viongozi wa Bunge wakiwa katika mazoezi ya vitendo juu ya Uongozi.Kushoto ni Bi.Maria toka Uingereza akiendesha zoezi la 'Leading by Example. Picha na Saidi Yakubu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Baada ya hayo mafunzo wakipewa jaribio 60% watapata Div 0, bisha!

    ReplyDelete
  2. Kwetu sisi mafunzo na vitendo tofauti kabisa. Injinia hawawezi kufanya mambo kama ujenzi, Spika hawezi kuacha unazi, Prof. wa uchumi hawezi kubadili uchumi, ..... yaani listi ni ndefu.

    Diploma, Degree, Semina, Kongamano, warsha, ziara za mafunzo hazileti mabadiliko kwetu hapa Tanzania.

    Mdau
    Makini

    ReplyDelete
  3. Sibishi kabisa mtu wangu,naungana na wewe

    ReplyDelete
  4. Haaaaah!Hii kali....na mahasira yao yatawekwa wapi?

    Inashangaza . Lakini ni vema mchawi ukimkabidhi mtoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...