Picha na habari na Faustine Ruta, Bukoba

Wakati msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa  uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 570 BYU lilowabeba Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu na kutaka kuungua.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari hilo. 

Mara baada ya dereva kugundua kuwa gari analoendesha linataka kuungua alilisimamisha  na kuwaambia abiria wake kuwa gari linaungua.
Kwa mujibu wa wabunge waliokuwemo kwenye gari hilo, baada ya kuambiwa kuwa gari linaungua kila mmoja alifanya juhudi za kujiokoa, wengine wakipitia madirishani.
Kwa Bahati hakuna Mbunge aliyeumia isipokuwa Mhe. Batenga  aliumia mkono kidogo baada ya kubanana sana mlangoni. 


Baada ya kila mmoja kutoka gari hilo liliendelea kutoa moshi mzito sana lakini kwa  halikushika moto na baadae lilizimika na kuacha kutoa moshi.

Wabunge waliokuwemo katika gari hilo ni Rebbecca Mngondo (Arusha Viti Maalumu), Rita Kabati (Iringa Viti Maalumu), Mariam Msabaha (Zanzibar Viti Maalumu), Mhe. Batenga (Kagera Viti Maalumu), Mhe. Madabida (Dar es Salaam Viti Maalum), Clara Mwatuka (Mtwara  Viti Maalumu).
Wengine ni Mzee Hussein (Zanzibar), Mussa Haji Kombo (Pemba Zanzibar), Abdul Mteketa (Jimbo la Kilombelo), Mutula Mutula (Jimbo la Tunduru Kusini). 

Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Peter Serukamba Hakuwemo katika gari hilo lilotaka kuungua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hawa ni wepi?katika wale kumi waliomwagwa?

    ReplyDelete
  2. Moshi mweupe ni ishara ya papa kutembelea hapo teh teh teh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...