Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo leo jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Usawa na Uwezeshaji wa Wanawake leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwemo waheshimiwa Majaji wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa warsha hiyo ya siku 1.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) , mama Salma Kikwete (kulia) akiagana na viongozi wa Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania mara baada ya kufungua wa warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.
Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamani tuwe wakweli tu lakini Mama Salma anapendeza sana, seriously toka amekuwa first lady, sijawahi kuona picha hata moja amevaa vibaya, au marangi rangi ya ajabu. She knows how to dress from head to toe, mimi binafsi ninamsifu, na kumu admire and as a woman truly i feel so proud kuwa na first lady anayevutia na kupendeza namna hii; hongera mama Salma! Hope itakuwa ni mfano wa kuigwa kwa first ladies watakaofuata.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa Kwanza,

    Hata mimi nakuunga mkono kwa Kauli hiyo, pia ni muhimu akina mama hawa ambao ni mifano mizuri Mama Salma Kikwete, Mama Bilal Mama Pinda na wengineo wengi wawe wanaalikwa ktk Hafla za wasichana hasa hawa Ma-Miss ili angalau wasichana waone mifano mizuri na kujirekebisha!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...