Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi

Jumla ya watuhumiwa 32 wa unyang'anyi wa kutumia silaha na wahamiaji haramu 6809 wamekamatwa kufuatia operesheni kimbunga ya kuwasaka majambazi, watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na kuwaondoa wahamiaji haramu inayoendelea katika mikoa mitatu Kigoma, Kagera na Geita hapa nchini.

Akizungumzia operesheni hiyo Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Simon Siro alisema kuwa operesheni hiyo ilifanyika na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji Hao haramu wakiwemo wanyarwanda 1446, warundi 4229' na waganda 647.

Wengine ni wakongo 443,wasomali 42, Myemeni1 pamoja na mhindi 1 Alisema kuwa operesheni hiyo pia ilifanikisha kukamata silaha 22 zikiwemo bunduki nne (4 ) za kivita aina ya SMG, gobole 15 ,shot gun moja(1)mark iv moja (1)na risasi za bunduki za kivita SMG na SAR 265 mark iv 20 na risasi za gobole 82 , Pamoja na mitambo miwili (2) ya kutengenezea magobole.

Aidha, aliongeza kuwa katika operesheni hiyo walifanikiwa kukamata mabomu sita(6) ya kurusha kwa mkono pamoja na nyara za Serikali.

Alibainisha nyara hizo kuwa ni ngazi ya Duma mmoja(1), ngazi mbili za Swala na magogo 86 pamoja na vipande kumi (10) vya nyama vinavyodhaniwa kuwa ni vya nyara za Serikali.

Kamanda SIro aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa zozote za uhalifu, wahamiaji haramu, na watu wanaowajua kuwa wanamiliki silaha kinyume cha Sheria ili waweze kukamatwa na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hahahaha Serikali si mchezo!

    Ehhh jamani, Wahamiaji Haramu walikuwa wanaishi kwa Bahati tu na sasa Bosi (Serikali) amekasirika wanatafuta njia za makwao!!!

    ReplyDelete
  2. Wageni Haramu walikuwa wanaishi kwa Rushwa tu, na sasa Kiama chao kimewadia!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...