WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teklonojia, Profesa Makame Mbarawa akikagua  eneo ambalo mwanachi mmoja wa kijiji cha Magaoni aling'oa waya wa mkonga wa Taifa.
 WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teklonojia, Profesa Makame Mbarawa na maafisa wa TTCL mkoa wa Tanga wakiangalia sehemu ambayo mwananchi mmoja wa kijiji cha Magaoni ameng'oa mkongo wa Taifa kwa sababu anazozijua mwenyewe
 wafanyakazi wa TTCL akiwemo ofisa habari wa Wizara hiyo Bi Prisca Ulomi (kulia) wakimsikiliza waziri akizungumza nao.
Waziri akiagwa na wafanyakazi wa shirika hilo mjini Tanga


Picha na Habari na 


Mashaka Mhando,Tanga
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teklonojia, Profesa Makame Mbarawa, amelitaka shirika la Simu nchini (TTCL), kufanya matengenezo ya haraka endapo Mkonga wa Taifa wa mawasiliano utapata hitilafu au kuhujumiwa na baadhi ya wananchi ambao hawajui umuhimu wa kulinda rasilimali za Taifa ili wasilete usumbufu kwa watumiaji wake.
Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wale wa Posta Jijini Tanga, Waziri Mbarawa alisema ni vema shirika hilo likatambua umuhimu wa mkongo huo kwa faida za kiuchumi kwa mafundi kuchukua hatua za haraka na za muda mfupi kufanya marekebisho kuliko kuchukua muda mrefu unaokera watumiaji.
Alisema zipo sehemu nyingine mkonga huo unapoharibika, mafundi huchukua takribani wiki mbili kukamilisha matengenezo hayo hatua ambayo alisema haina tija kwa ufanisi kutokana na kwamba mkonga huo kiuchumi umekuwa ukisaidia na kwamba serikali imetumia fedha nyingi katika kuuchimbia na kuuendesha kwake.
Akizungumzia 'ndoa' ya shirika hilo na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, Waziri Mbarawa alisema serikali inafanya mchakato wa kuvunja mkataba huo ili shirika hilo la TTCL liweze kujiendesha wenyewe tofauti na sasa.
Alisema hivi saa serikali kupitia Wizara ya Fedha (Hazina), inapitia na kufanya tathimini ya mali ya kampuni hiyo kabla ya kuvunja mkataba huo rasmi ili shirika hilo liendeshwe na wazawa wenye na serikali kuwekeza fedha kwa ajili ya uendeshaji na hatua iliyofikiwa ni kutangaza nafasi za juu za uongozi.
"Kuweni wavumilivu muda si mrefu tutamaliza suala hili lililokaa kwa muda mrefu, Hazina wanafanya tathimni kuangalia mali yao ikiwezekana TTCL isimame yenyewe kwa kuendeshwa na wazawa na serikali iweze kuweka mtaji wake," alisema Profesa Mabarawa.
Aliwataka wanyakazi na menejementi ya shirika hilo, wakawakisubiri suala hilo kukamilika na kuvunjwa, washirikiane na kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazoikabili shirika hilo ikiwemo ushindani na makapuni mengine ya simu yaliopo hapa nchini.
Awali meneja wa TTCL mkoani Tanga Bw. Peter Lusama aliwmeleza Waziri kwamba shirika hilo mkoani Tanga, linakabiliana na changamoto zilizopo ikiwemo kushughulikia matatizo ya uharibifu wa mkonga huo ambao alitoa mfano mwananchi mmoja wa Kijiji cha Magaoni wilayani Mkinga mkoani hapa, alipokuwa kitafuta mchanga kwenye kichuguu, aling'oa kipande cha mkonga huo.
Hata hivyo, alipoeleza kwamba mafundi kutoka Dar es salaam walichukua zaidi ya masaa 36 kukamilisha matengenezo hayo, hatua ambayo Waziri huyo aliona kwamba haikuwa na sababu ya kuchkua muda huo wote na kuagiza mafundi wachukue muda mfupi kukamilisha kazi hizo.

Waziri Mbarawa alikuwa mkoani Tanga kutembelea mkonga wa Taifa wa mawasiliano katika eneo la Horohoro ambako tayari mradi huo ulikamilika tangu Juni 2012 kisha kuzungumza na wafanyakazi kujua changamoto zao na kuwaagiza kufanya kazi kukabili changamoto hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hawa Wahalifu wa Miundombinu ya Tekinolojia wanastahili adhabu kali sana.

    Sisi tunapigania maendeleo kuipita Karne ya 21 wao wanaturudisha nyuma kuelekea Karne ya 12!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...