Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu  ya mwanafunzi  na ufaulu jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mr President please angalia hawa wamefuta alama ya sifuri kwa sababu za Kisiasa na kuficha haibu kama iliyotokea kipindi cha nyuma!!

    Angalia wanatuaribia elimu ya Tanzania.

    Wadau wa elimu ingilieni Kati, Watanzania ingilieni kati, Wazazi ingilieni kati maana watoto wenu wanatengenezwa kuwa maboya!!

    eti division V!! ata aibu hamuoni!!

    ReplyDelete
  2. Hii ni hopeless kabisa hakuna maana kusoma sasa. Unasoma ili uwe nani? hivi hawa ni watanzania waliofanya hivi au ni wageni wa nchi? nafikiri watanzania hawawezi kufanya namna hii jamani. Hebu tuone aibu kwa hili. USA tunanyanyasika alama A+ ni 95-100, A- ni 94-90, B+ 87-89, B ni 83-86, B- ni 80-82, C+ ni 77-79, C ni 73-76, C- ni 70-72, D+ ni 65-69, D ni 60-64, F ni 59-0. Hebu imagine sisi 59 ndo B or C. hakika miaka ijayo hakutakuwa na wasomi kabisa mtanambia. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. shame on you all who made these decisions!

    JK please do something Sir!

    ReplyDelete
  4. Mh Mbatia, Zitto Kabwe na wengineo mpo wapi???!! Mbona mnakaa kimya nchi inaenda kombo hivi???!!

    Mtakiambia nini kizazi kijacho wakati tunawaachia wachache watibue elimu ya Tanzania!!??.

    ReplyDelete
  5. Nimesoma moaning yenu wote lakini sikubaliani na div v. Pia mdau unayelinganisha na usa huo si uumngwa kabisa! Huko USA watoto wameshiba, hawatembei, vitabu, walimu wa kutosha. Anyway. It's painful

    ReplyDelete
  6. Kwa Mpango huu mpya ni kuwa:

    ''HAKUNA KUFELI''

    Pia aliyesoma na asiyesoma ni sawa sawa.

    Ohhh Elimu nchini Kwishneyyy!!!

    ReplyDelete
  7. Wakenya walikuwa wanatudharau lakini kwa Mtindo wetu wa National Exams walikuwa wanatu heshimu kwa kuwa ukiingia kwenye Mtihani ukitereza UNAPATA DIVISHENI ZERO NA CHETI HUPATI!

    Wanafunzi wa Tanzania sasa watapata muda mzuri wa ku chat na simu zao badala ya kujipinda na masomo.

    WAKATI WAO KENYA VILAZA WAO WANAINGIA KTK VYUMBA VYA MITIHANI WANAANDIKA MAJINA NA NAMBA KTK VITABU VYA MAJIBU WANAPATA GRADE 4 AMBAYO CHETI UNATAPA LAKINI NDIO DARAJA LA MWISHO KWA TANZANIA SAWA NA DIV ZERO !

    ReplyDelete
  8. Mdau wa 5 upo sahihi ni vema ndugu yetu Clara Manyalila Mtoa Maoni wa 2 asifananishe Madaraja ya Masomo ya Elimu ya Marekani wanakotumia DIGITAL LIBRARIES, NEW ORDER OF LEARNING, IT-BASED EDUCATION SYSTEMS na Tanzania ambako watu bado wangali ktk zama za gizani Kusoma kwa kukesha miguu ikiwa ndani ya ndoo za maji!!!

    ReplyDelete
  9. Hawakupambanua umuhimu wa elimu bora kwa watanzania.

    Ni wazi kuwa watoto wa waliopitisha sera hii hawategemei kupata elimu ya hapa nchini.

    Aibu yao!!!!!

    ReplyDelete
  10. Kwa hali hii ya elimu, sioni sababu kwanini tunalalamika tunapotengwa katika mambo mazito yanayohusu Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Wenzetu wameshatuona jinsi tusivyo na akili na tunazidi kuonyesha ujinga wetu na kuweka hadharani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...