Sekretarieti
ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki ilifanya kikao cha pili cha baraza la
wafanyakazi wake ambapo kwa mujibu wa katibu wa baraza hilo Ndugu Paul Masanja
wajumbe wa baraza hilo ni pamoja na wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Ofisi zote za Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Dodoma, Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Dodoma na Uongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na Afya
TUGHE Mkoa.
Masuala
muhimu katika kikao hiko cha baraza la wafanyakazi yalijumuisha Nafasi ya vyama
vya wafanyakazi ndani ya baraza hilo, masuala ya mafao kwa watumishi wa Umma.
Vilevile mapitio ya bajeti ya mwaka 2012/13, bajeti ijayo ya 2013/14 na kupitia
mtiririko wa bajeti kwa kipindi cha kuanzia 2009/10 hadi 2013/14.
Mgeni
rasmi katika kikao hiko alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
ambapo miongoni mwa masuala aliyoyapa msisitizo katika salamu zake za ufunguzi wa
kikao hiko ni pamoja na yafuatayo:
·
Sera ya “Tenda kwa matokeo makubwa
sasa” (Big Result Now). Dr. Nchimbi aliwataka watumishi wa umma kwa nafasi zao
kwenye ofisi za serikali na shughuli mbalimbali lazima wajiwekee vipaumbele vya
majukumu yao na kuweka mkakati mzuri wa utekelezaji utakaoleta ufanisi mkubwa
na kasha kuweka utaratibu wa kupima matokeo ya utendaji.
Alifafanua
kuwa lazima wafanyakazi waweke vipaumbele vinavyolenga kuleta mabadiliko
makubwa katika kutatua kero na changamoto za wananchi mfano kwenye sekta ya
utunzaji kumbukumbu/masijala, Afya na sekta zingine za huduma na uzalishaji.
·
Dr. Nchimbi aliwataka
watumishi/wafanyakazi hususani wataalamu wa kilimo kujadili na kutafuta
ufumbuzi wa pamoja wa tatizo la muda mrefu la upungufu wa uzalishaji wa chakula
ndani ya mkoa unaoleta tatizo la upungufu wa chakula mara kwa mara mkoani
Dodoma ukilinganisha na mahitaji ya chakula yaliyopo kwa hivi sasa.
·
Vilevile aligusia
tatizo/changamoto ya Mkoa wa Dodoma kuwa na matokeo yasiyoridhisha katika sekta
ya elimu hususani ngazi ya msingi na sekondari. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa Dr.
Nchimbi, wafanyakazi wanaujuzi na utaalamu katika nyanja mbalimbali kulingana
na mahitaji hivyo hawana budi kutumia utaalamu na ujuzi wao wote kusaidia Mkoa
wa Dodoma kuondokana na tatizo lao la kufanya vibaya kwenye sekta ya elimu.
·
Msisitizo mwingine uliwekwa
kwenye suala la kuboresha hali ya makazi ya wananchi/ujenzi wa nyumba bora za
makazi za wananchi na uondoshaji wa Tembe. Wataalamu wawasaidie wananchi
kuboresha shughuli zao za uzalishaji na kujiwekea utaratibu wa kufanya mavuno
kwenye shughuli zao hususani kuvuna mifugo na mazao na kuwekeza kwenye
kuboresha makazi yao kuanzia ngazi za vijijini hadi mijini.
·
Dr. Nchimbi
aliwatahadharisha watumishi wa Umma wenye tabia ya kuhujumu serikali wawe
makini, aidha alikemea mahubiri hasa ya siasa yenye viashiria vya uvunjifu wa amani, utulivu na
mshikamano, vurugu na umwagaji damu; aliwaasa watumishi/wafanyakazi wasikubali
kujihusisha na suala hili. Badala
yake watumishi wa umma wanatakiwa kuzingatia maadili mema ya kazi zao,
kuzingatia taratibu, kanuni na sheria ili kuboresha utoaji wa huduma katika
sekta zote.
·
Vilevile Dr. Nchimbi
aliwasisitiza wafanyakazi waone umuhimu wa kijiendeleza kielimu ili kuzidi
kuboresha utoaji wa huduma zao na utendaji wao kwa ujumla. Aliwataka
wafanyakazi watumie fursa zilizopo kama vile vyuo kujiendeleza. Aliwaagiza
waajiri (Katibu Tawala Mkoa) kutoa kipaumbele cha ruhusa kwa ya kusoma kwa
watumishi wa serikali wanaotaka kujiendeleza kielimu kupitia chuo kikuu huria
cha Tanzania tawi la Dodoma kwa kuwa hawaaribu ratiba ya kazi kwani wanaweza
kusoma huku wanafanya kazi kuitumikia serikali.
Alikemea
tabia ya watumishi/wafanyakazi wasiopenda kujiendeleza kielimu kwa kubakia
kwenye daraja moja la elimu kwa muda mrefu bila kujiendeleza na kusema kuwa
inazorotesha utendaji na ufanisi.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa baraza hilo la wafanyakazi wa sekretarieti ya Mkao wa
Dodoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa
Mkoa Dodoma Ndugu Rehema Madenge alitoa Rai kwa wafanyakazi wa serikali wawe na
desturi ya kubadilika kuanzia sasa na kusisitiza alichokieleza mkuu wa mkoa
hususani sera ya Tenda kwa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now).
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma
Idara ya Habari