Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha CCM,Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na wananchi/Wanakijiji wa kijiji cha Ilala Simba kilichopo Kata ya Nzihi,Iringa Vijijini mapema leo jioni,alipokwenda kuzungumza nao na kuomba ridhaa yao ya kuwaongoza kama Mbunge.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha CCM,Godfrey Mgimwa akizungumza na Wananchi/Wanakijiji wa kijiji cha Ilala Simba kilichopo Kata ya Nzihi,Iringa Vijijini mapema leo jioni,akiomba kura na ridhaa yao ya kuwaongoza kama Mbunge. Ndugu Mgimwa alisema kuwa Wananchi Wamuamini kwani anafahamu changamoto zilizopo na majibu ya kuzitatua anayo "Nimefanya utafiti  wa kutosha hivyo najua changamoto zinazotukabili,nipeni nafasi ili niweze kuzitatua kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010" alisema Mgimwa.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa,Mh.Gervas Ndaki akiwa amepiga magoti ikiashiria kutoa heshima kwa wananchi kwa ajili ya kuwaomba kura kwa ajili ya Mgombea wa CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika kijiji cha Ilala Simba kata ya Nzihi mkoani humo.
 Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Ilala Simba kilichopo Kata ya Inzihi,Iringa Vijijini,wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mapema leo jioni.
 Wanachama wa chama cha CCM na wananchi wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanywa na CCM mapema leo jioni,ambapo mgombea wa chama hicho,Godfrey Mgimwa alifika na kujinadi kuomba kura na ridhaa ya kuongoza jimbo hilo.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha CCM,Godfrey Mgimwa akipokelewa kwa shangwe mapema leo jioni katika kijiji cha Magubike,kabla ya kuzungumza nao kwenye mkutano wake wa hadhara,katika safari nzima ya kuomba kura na ridhaa ya kuwaongoza kwa nafasi ya Ubunge.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mapema leo jioni katika kijiji cha Magubike,ikiwa ni sehemu ya kumnadi mgombea wa chama hicho,Ndugu Godfrey Mgimwa ambaye anagombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kalenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...