Nimepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni ikidaiwa ni mawasiliano baina yangu na Ridhiwani Kikwete, Mjumbe wa NEC na Mbunge mteule wa Jimbo la Chalinze.

Ingawa si tabia yangu kukanusha mambo yaliyotengenezwa kwa sababu anazojua muandaaji lakini kwa idadi ya simu nilizopokea kwa faida ya wengi ni bora niseme yafuatayo.

1.Kwa wanaofahamu matumizi ya whatsapp, screen shot hii ilipaswa kutoka kwenye simu yangu, kwa maana nyingine ni mimi mwenyewe ndiye chanzo cha jambo hili.

2. Wanaonifahamu whatsapp sio moja ya njia yangu ya mawasiliano, situmii simu aina ya samsung ambayo ndiyo inayoonekana ilikuwa inatumika katika mawasiliano hayo,na pia siifahamu na wala sijawahi kuwa na namba ya Airtel ya Ridhiwani.

3. Ukiiangalia Lugha na aina ya uchaguzi wa maneno uliotumika si aina yangu ya uandishi na maneno hata ambayo huwa nayatumia katika mazungumzo ya kawaida,mtu yoyote anayejua siasa atatambua mazungumzo hayo hayana mantiki yanaongelea mambo mengi na watu wengi kwa wakati mmoja.

4.Tarehe 5 April nilikuwa kwenye hall of fame Chuo kikuu Mzumbe na si Chalinze nilikokuwa tarehe 2,3 na 7. Muda wa ujumbe unatofautiana sana 5 am, 6.30am na 2.32pm.

Screenshots zinaonyesha kwamba majadiliano hayo yalifanyika tarehe 5 April ambayo mimi nilikuwa tayari Chuo Kikuu Mzumbe.

Mimi niliondoka Dar kwenda Chalinze rasmi siku ya tarehe 2 nikitokea katika shughuli za ugawaji wa madawati katika shule ya Sekondari Pugu  ambapo nilikuwepo huko tangu asubuhi bila kupitia sehemu yoyote na niliongozana na MNEC Anthony Mavunde kwa kupitia njia ya kisarawe ili kukwepa foleni. Na tarehe 7 nilienda tena Chalinze kusherehekea ushindi.

5. Jambo hili ni rahisi sana kulitengeneza kwa simu mbili na kusave majina unayotaka na unawezo hata wa kutoa ya upande wa pili inayoonyesha jina langu.Matumizi haya ya teknolojia ni vyema yatumike katika mambo ya msingi badala ya kujaribu kuleta fitna zisizo na maana na kujaribu kuwapa watu tabia ambazo hawajawahi kuwa nazo.

6. Ushauri wangu ni kwa kila mmoja wetu hasa wanasiasa kuwa makini na kuepuka kufitinishwa kwa fitina nafuu kama hii. Kwa jambo lilozungumzwa kwanza wakati bado na pili wanasiasa wa ngazi yangu na Ridhwan si wakulijadili jambo kubwa namna hiyo kwa hoja dhaifu hivyo na tena  kwenye whatsapp.

-JERRY SILAA.

Source ya majibu ni facebook page ya Jerry Silaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sijui hayo anayozungumza lakini nataka kumwelewesha Ridhiwani sio mbunge mteuliwa, amechaguliwa kwa kupigiwa kura na watu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa appointed na kuwa elected. Kama kiongozi anatakiwa ajue tofauti hizo kwasababu kama angekua ni wa chama tofauti na Ridhiwani ningefikiria ana lake jambo kwa kumuitwa mteuliwa. kwa kifupi angesema mbunge mpya wa Chalinze ingeeleweka.

    ReplyDelete
  2. Mhe. jerry Silaa umeongea suala nyeti sana na linalo wagharimu watu wengi sana.

    Pana umuhimu masuala haya mawili (i)La Vitambulisho vya Utaifa vyenye uwezeshaji wa Kieletroniki, (ii) Sheria ya Makosa ya Mtandao /CYBER CRIME ACT) vipatikane haraka ili tuweze kuepekana na matatizo kama haya.

    Hayo mawili yakitimia, tutaweza kusajili namba za simu na komputa zetu kwa umakini na sioyo holela kiasi cha mtu kuweza kuposti Taartifa kwa jina la mwingine kama hapo ulivyosema.

    Pia tuweze kudhibiti Taarifa zetu za siri hadi za Kifedha kwa kutumia hivyo viwili.

    Jamaa yangu mmoja alishangaa sana kukuta Masuala yake ya Kifedha Benki (hadi idadi ya fedha anazomiliki Benki) yanafahamika na watu fulani anao fahamiana nao kumbe hao jamaa zake wana fuatilia kwa siri Akaunti zake za Benki wakishirikiana na Watumishi wa Benki wasiokuwa waaminifu wakizitoa taarifa zake nje bila ridhaa yake!.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na jerry kwa asilimia mia moja. Ule ni upuuzi mtupu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...