Marehemu Mzee John Gasper Nshimba
1933 – 2014

Familia ya Marehemu Mzee John Gasper Nshimba wa Vingunguti, tunatoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki kwa hali na mali katika msiba wa baba yetu mpendwa Mzee John Gasper Nshimba aliyefariki tarehe 15/03/2014 na kuzikwa tarehe 17/03/2014 Segerea.

Kwa kuwa ni vigumu kutaja wote walioshiriki, shukrani za pekee zimfikie Paroko wa Parokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu – Vingunguti, Father Gasper Sung’hwa wa Arusha, wanajumuia wa Bikira Maria, ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nasi kwa hali na mali.

Mkesha wa arobaini ya Mzee John Gasper Nshimba utafanyika nyumbani kwake Vingunguti siku ya tarehe 25/04/2014 na misa tarehe 26/04/2014 katika kanisa katoliki Vingunguti saa moja asubuhi.

Bwana alitoa, bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...