Mkurugenzi wa Tanzania Horticulture Association (TAHA),Bi. Jackline Mkindi (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari ambao hawapo
pichani juu ya maonesho ya kilimo ambao yanatarijiwa kufanyika siku ya
Aprili 25 na 26 katika viwanja vya AVRDC vilivyopo eneo la Tengeru
wilayani Arumeru mkoani Arusha.kulia kwake ni Mratibu wa Agri-Hub
Tanzania Bw. Tom Ole Sikar.
Na Woinde Shizza,Arusha
WAKULIMA na wafanyabiashara za kilimo zaidi ya 500 kanda ya kaskazini
mwa Tanzania wanatarajiwa kukutanishwa na taasisi za kifedha 48 ili
kuweza kuongeza ufahamu na uelewa juu ya huduma mbalimbali za kifedha
zitolewazo na mabenki,taasisi ndogo ndogo za kifedha,mashirika ya
bima,taasisi za elimu na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza na vyombo vya habari,Afisa mtendaji mkuu wa TAHA,Jackline
Mkindi alisema kuwa wakulima wadogo wadogo wamekukwa wakikabiliwa na
changamoto kubwa ya ya upatikanaji wa huduma za kifedha hususani kwa
wadau wa sekta ya kilimo.
Katika kutatua changamoto hiyo ya mitaji Agri-Hub Tanzania
ikishirikiana na TAHA mashirika,asasi mbalimbali kwa umoja wao
wamethamiria kuwaunganisha wadau wa kilimobiashara na watoa huduma za
kifedha moja kwa moja ili pande zote mbili ziweze kukuelewana na juu
mahitaji yao na hatimaye watoa huduma za kifedha waweze kubuni huduma
bora zaidi za kuimarisha utoaji huduma zao kwa wadau wa kilimo.
Mkindi alisema kuwa maonesho hayo yatakwenda sambamba na uwasilishwaji
wawa mada mbalimbali ikiwemo uaandaaji bora wa wa mpango biashara
(business plans),umuhimu wa wa soko la hisa katika kuhakikisha
upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu na matumizi bora ya mikopo katika
biashara hususani za kilimo.
Naye mtaribu kutoka kampuni ya Agri-Hub Tanzania Tom Ole
Sikar,alisisitiza kuwa maonesho hayo yanalenga kuwawezesha wakulima
wajasiriamali pamoja na wamiliki wa biashara za kilimo kama
wachuuzi,wauzaji wa pembejeo na wasindikaji kutambua fursa mbalimbali
za mitaji na usalama wa kifedha(Financial security) zilizopo kwa
biashara za kilimo.
Aidha sikar alisema kuwa wadau hao wataweza kuunganishwa na taasisi
muhimu za fedha ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mawasilisho na
majadilino juu ya fursa za sekta binafsi katika kilimo pamoja na
wataalamu wa mambo ya fedha na watoa huduma za maendeleo ya biashara
kupitia semina zitakazotolewa sambamba na maonesho hayo.
''maonesho hayo yatawawezesha wadau kutambua njia za kuboresha
biashara na utoaji wa huduma kwa walengwa ikiwa ni pamoja na kujifunza
kutoka kwa wafanyabiashra wengine wa kilimo waliofanikiwa kutembelea
maonesho "alisema bw,Sakar.
Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Taasisi ya
AVRDC(The World Vegetable Centre) kuanzia tarehe 25 na 26 april
kuanzia majira ya saa tatu aubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...