Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo ya muda mfupi, Chuo cha Diplomasia kimeendesha mafunzo ya juma moja ya Itifaki na Uhusiano ‘PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS’ 
Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi. Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo ya muda mfupi yatolewayo na Chuo cha Diplomasia, mathalan usuluhishi na utatuzi wa migogoro (Conflict Resolution and Mediation skills) na Itifaki na Uhusiano ( Protocol and Public Relations)
Mafunzo hayo yalihusisha maofisa wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali na sekta binafsi kama Benki Kuu ya Tanzania, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Meya Kinondoni, NSSF, Idara ya Uhamiaji, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Umoja wa Mataifa (UN) na Clouds Media.
Mafunzo hayo ya juma moja yaliyofanyika Kurasini Dar es salaam, washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma.
Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bw. Juma M. Kanuwa alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wa kazi zao. 
“Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa umma (Protocol and Public Relations) zinahitaji utaalam ambao utamfanya mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo mazuri. Hivyo mafunzo haya ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa na Chuo cha Diplomasia yana lengo la kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupata matokeo bora,” alisema.

Akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji mafunzo haya  yatarudiwa tena Tarehe 18 -22 Agasti 2014 hapa chuo cha Diplomasia, na kuwataka wale wote wanaohitaji wafike chuoni ama kupiga namba 0713667303 kwa maelezo zaidi na kupewa utaratibu.

Kwa kawaida wawezeshaji wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika Chuo cha Diplomasia, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao. 
Mshiriki Baby Kabaye wa Clouds Media akionesha cheti chake kwa furaha
Mshiriki Godfrey Makupa wa GRM Productions akifurahia cheti chake
Washiriki wakiwa darasani
Mshiriki Baby Kabaye wa Clouds Media akifafanua jambo.
Imetolewa na Shoo Innocent, Afisa Uhusiano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...