Shirika la AGPAHI ni shirika la Kitanzania linalofanya kazi ya kutokomeza UKIMWI na kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa watoto. AGPAHI ilianzishwa kwa msaada wa Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) mwaka 2011kwa lengo la kutokomeza UKIMWI kwa watoto wachanga nchini Tanzania.

AGPAHI na EGPAF ni mashirika mawili yanayojitegemea na ni washirika kupitia makubaliano baina yao. AGPAHI inafanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania katika kusaidia kutoa huduma za kinga, matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na VVU katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita.
 Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF), Charles Lyons (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Laurean Bwanakunu wakati alipotembelea ofisi  za shirika hilo zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam, kuangalia maendeleo yake tangu lianzishwe mwaka 2011. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa EGPAF Tanzania, Jeroen Van’t Pad Bosch. 
Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF), Charles Lyons akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa AGPAHI.
 Viongozi wa Shirika la EGPAF wakiwa katika mkutano na baadhi ya wafanyakazi wa AGPAHI. 
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa mkutano na Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la EGPAF, Charles Lyons aliyetembelea ofisi za shirika hilo hapa Dar es Salaam.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la EGPAF, Bw. Charles Lyons (kushoto) akiondoka katika ofisi za AGPAHI, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Bw. Laurean Bwanakunu.Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa AGPAHI, Dk. Amos Nsheha na Mkurugenzi wa EGPAF Tanzania, Jeroen Van’t Pad Bosch. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...