10349153_841207622565532_7288991937464718532_n
Unaweza kuwa humfahamu kwa vile hana kelele nyingi....TUONYESHE UZALENDO KWA KUMPIGIA KURA SASA.

Msanii bora wa muziki wa Reggae Tanzania, DABO (Pichani) amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa, baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa kabisa za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (International Reggae and World Music Awards (IRAWMA).
DABO anawania tuzo hizi katika kipengele cha Mtumbuizaji Mpya Bora, akikabiliwa na ushindani kutoka kwa wasanii MC Norman kutoka Uganda, Alkaline na Kranium kutoka Jamaica na Shatta Wale kutoka Ghana.
196441_588093307897900_104541301_n
Zoezi la kuwapigia kura wasanii hawa kuwawezesha kushinda linaendelea sasa mtandaoni. Link ya kumpigia kura ni: http://www.irawma.com/irawma_vote2014
DABO ametajwa kuwania kipengele cha Best New Entertainer
Kwenye kipengele hicho, DABO anachuana na
* Daniel Bambatta Marley - Jamaica
* MC Norman - Uganda, Africa
* Alkaline - Jamaica
* Kranium - Jamaica
* Shatta Wale – Ghana
Asante kwa Kuunga mkono zoezi zima ndio kama linaanza!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Asante Ankal
    Nashukuru kwa kupitia wall yangu....

    ReplyDelete
  2. Ankali, Video tafadhali ya huyu msanii wetu maana bila video tunapiga kura bila ufahamu wa kutosha.

    ReplyDelete
  3. Dabo - Interview 2012 Carribean Beat http://www.youtube.com/watch?v=uROhT8fD73o

    ReplyDelete
  4. Sawa, Nimemkubali,sasa baada ya kuona video ya Dabo kura nyangu ya ndiyo naipiga sasa kwa msanii huyu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...