Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI Reuben de La Red amefunga mabao matatu peke yake, wakati
magwiji wa Real Madrid wakiiangusha Tanzania Eleven 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam leo.
De la Red
alimfunga bao moja kipa Mwameja Mohamed kipindi cha kwanza na kipindi cha pili
akamtungua mara mbili Manyika Peter, wakati bao pekee la Stars lilipatikana
baada ya Real kulijifunga wenyewe kupitia kwa Roberto Rojas.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi mpira uliotumika De La Red baada ya kuutia
saini yake juu yake, kabla ya kuwakabidhi Kombe Real Madird kwa ushindi wao
huo.
Katika mchezo huo, ambao wachezaji waliingia na
kutoka, Real Madird walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, kupitia kwa De
La Red ambaye alimalizia pande tamu la Luis Figo.
Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa kiungo Christian Karembeu,
aliyezuia shambulizi la Tanzania na kuanzisha shambuizi zuri lililozaa matunda,
akiuvuka msitu wa wachezaji wa wenyeji kwa umahiri mkubwa.
Tanzania Eleven ilisawazisha dakika ya 45 baada
ya kona ya Mecky Mexime kuzua kizaa langoni mwa Real na Roberto Rojas
akajifunga katika harakati za kuokoa baada ya Kali Ongala kuuparaza kwa
kichwa.
Kipindi cha pili, De la Red alifunga bao la pili
kwa penalti dakika ya 81 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Habib Kondo
kwenye eneo la hatari.
Awali ya hapo, Figo alimtoka vizuri beki Mecky
Mexime na kuingia hadi kwenye eneo la hatari akiwa kwenye nafasi ya kufunga
akampasia De La Red ambaye alipiga nje.
De la Red alikamilisha hat
trick yake dakika ya 88 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Tanzania
Eeleven.
Wachezaji wa timu zote mbili
wanatarajiwa kula chakula cha usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu baadaye leo.
Luis Figo akimtoka Athumani China |
Beki wa Tanzania, Nsajigwa Shadrack kushoto akimtoka Fernando Sanz wa Real Madird |
Reuben De La Red kushoto amefunga mabao matatu peke yake Real ikishinda 3-1 Uwanja wa Taifa
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Real Madrid Legends. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
|
Sio mbaya tujipange nasi tukienda kwao tuwapige 6 kwa nunge
ReplyDeleteWakongwe wameperfom kuzidi starz
ReplyDeleteMm nashauri tim yao ya wakongwe wasiivunje kila likitokea tamasha wawe wanacheza itawasaidia kuwa na mazoezi na vile vile upendo vile vile kama watakuwa na mfuko maalum kwa wachezaji wastaafu ikiwa moja wao kapata matatizo utawasaidia
ReplyDeleteHow wrong can one be.Niliposikia ni wakongwe nilidhani kuwa ni vibogoyo na wana mikongojo.
ReplyDelete