Na   Magreth Kinabo, Dodoma

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho  Kikwete ameahidi kuonana na Viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demkrasia Tanzania(TCD) kabla ya mwisho wa wiki kwa lengo la kushauriana.

 Kauli  hii imetolewa na Mwenyekiti wa TCD,Mhe. John  Cheyo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi  wa   katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Bunge.

Mhe. Cheyo alisema Rais Kikwete amekubali kuonana nao kufutia kikao chao walichokaa kwa pamoja ambacho kilihusisha viongozi  wakuu wa vyama hivyo, Agosti 23,mwaka huu, ambapo walijadili na kutafakari maendeleo ya mchakato wa Katiba Mpya.

Alisema viongozi hao, katika kiako hicho cha  pamoja na mambo mengine waliazimia kutafuta nafasi ya kuonana na Rais Kikwete kwa  ajili ya lengo hilo, ambapo kufutia azimio hilo, Mwenyekiti huyo aliwasiliana  naye  alilipokea  azimio  hilo na kuahidi kufanya hivyo.

“Tutalishauri taifa kwa maoni tutakayokubaliana na Rais,” alisema Mhe. Cheyo bila ya kutaja agenda  juu ya jambo hilo.

Aliongeza kuwa  watazunguza na kutafakati ili  kuhimarisha amani na mchakato huo utoe matunda mema.

Mhe. Cheyo alisema kikao hicho kilifanyika na kuhusisha vyam vyote vilivyoko  katika TCD.

Alisema hii ni mara ya kwanza kwa TCD  kumwomba Rais Kikwete kuonana naye na kukubali ombi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...