Afande Sele akiwa na watoto wake wawili alioachiwa na Marehemu Mama Tunda,ambao ni Tunda na Asante Sanaa wakiwa wamepozi mbele ya Camera ya Globu ya jamii mapema leo mchana,Walipokwenda kwenye Arobaini iliyoanyika mtaa wa Amani mjini Morogoro.
 Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Mkali wa Rhymes Afande Sele akiushukuru Uongozi wa Clouds Media Group sambamba na kuwashukuru Wasanii hao waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu kufariki kwake.
 Afande Sele akizungumza kwa kuwataka wasanii kuungana na kuwa kitu kimoja katika shida na raha,kuacha tabia ya kubaguana na kujengeana chuki ambako kumekuwa ni sehemu ya kuufanya muziki wao na mambo yao mengi yasifanikiwe ipasavyo,Hivyo amewashauri wasanii kuwa na roho ya kupendana na kufanya kazi zao kwa kujituma na ubunifu ili tasnia ya muziki iweze kufika mbali zaidi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mo Music anaetamba na wimbo wake wa Basi nenda unaofanya vyema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini,akitoa mkono wa pole kwa Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana.
 Mtoto wa kwanza wa Afande Sele,aitwaye Tunda akisalimiana na baadhi ya wasanii waliofika kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mama mzazi wa marehemu Mama Tunda (aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Afande Sele),mtaa wa Amani mjini Morogoro mapema leo mchana,ambapo Marehemu Mama Tunda leo anatimiza siku arobaini tangu kufariki kwake.
 Baadhi ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakiwa na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa Familia ya marehemu Mama tunda,ambapo leo inafanyika arobaini yake,mtaa wa Amani mjini Morogoro.
PICHA NA MICHUZI JR-MOROGORO
PICHA ZAIDI INGIA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...