Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Watumishi wa Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro.

Wakicheza kwa kuonana timu hiyo ikiongozwa na Nahodha wao Carlos Mlinda walilisakama lango la wapinzani wao RAS Simiyu ambapo katika kipindi cha kwanza mcheza aliyevalia jezi yenye namba 11 Erick Mfugale aliwapatia goli la kuongoza kwa kipindi cha kwanza hadi mapumziko. Kipindi cha pili kilinza kwa timu zote kusaka ushindi ili kujihakikishia hatua inayofuata.

Dakika ya saba ya kipindi cha pili mchezaji aliyevalia jezi namba 8 Maurus Ndenda ndiye aliwanyanyua mashabiki wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufunga goli la pili kwa shuti kali na kuingia wavuni.

Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi wa mchezo huo Ramadhani Omari, timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeshinda 2 na RAS Simiyu hawajapata kitu ambapo ubao wa matokeo ulisomeka (Habari 2-Simiyu 0).

Aidha kwa upande wa mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo bahati haikuwa yao wamefungwa goli 39 kwa 10 na wapinzani wao Wizara ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waki wa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange dhidi ya RAS Simiyu leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Waamuzi wa mchezo mpira wa miguu kati ya timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na RAS Simiyu wakiongozwa na mwamuzi wa kati Ramadhani Omari (wa pili kulia) wote kutoka kituo cha michezo ya vijana chini ya miaka 20 kijulikaanacho kama Twalipo cha mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Agnes Mbambo akimiliki mpira wakati wa mechi yao na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenye mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro.
Wachezaji Johari Kachwamba (kulia) na Hadija Omari Jaa (kushoto) wakiwa kwenye harakati za kuwania mpira wakati wa mechi kati ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...