Mkurugenzi wa Lino Angency International Ltd Hashim Lundenga
Hivi karibuni kulifanyika mashindano ya kumsaka mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2014 (Miss Tanzania 2014) ambapo Sitti Mtemvu alitangazwa kuwa mshindi.
Baada ya kutangazwa huko, kukawa na mambo mengi yaliyosemwa kumhusu. Kuanzia tetesi za kuwa kadanganya umri mpaka elimu. Kuwa kuna rushwa ilitumika mpaka kusemwa ana mtoto.
Mkurugenzi wa Lino Angency International Ltd Hashim Lundenga, anazungumza na mitandai ya Vijimambo na Kwanza Production kuweka bayana
KARIBU


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. ANAJITAFUNA TAFUNA HAELEZI KINACHOELEWEKA. ETI KILA MTU ANADANGANYA....POLISI,ETC. KWA HIYO NDIYO JUSTIFICATION YA KUDANGANYA UMRI KWA SABABU FULANI AMEDANGANYA......HII MISS WORLD TANZANIA HAINA MAANA TENA, KUWA NA MAJAJI ALIOWACHAGUA YEYE SIYO SABABU YA KUSEMA MASHINDANO HAYANA UPENDELEO. BADO KUNA MAMBO MENGI YANAYOESHA UPENDELEO WA WAZI.

    ReplyDelete
  2. Bwana Hashim!
    Tunakubali kuwa uetumia cheti chakuzaliwa.
    Ila passport ipo wazi inayo onyesha umri tofauti kwahiyo ulitakiwa kuchukuwa hatua za haraka.
    tatizo hapo nikuwa inaonekana siti amedanganya.
    Na sio sawa kusema kuwa watanzania sio wastarabu wakati unashindwa kutatua swala dogo kama hili.

    ReplyDelete
  3. Lundenga tuletuletee passport orginal alio safiria kwenda marekani yenye visa ya marekani aliotumia akiwa huko kama kweli ile waliotoa wananchi wenye hasira na mafisadi kama wewe ni feki.

    ReplyDelete
  4. Ningekuwa Hashim haya yangekuwa majibu yenu.
    1. Paspoti si kigezo kwani si kila mwananchi ana paspoti sababu mamlaka huwapa paspoti wale tu wenye safari. Watu wengine hawajawahi kuwa na safari.

    2. Kuhusu cheti kimetolewa na mamlaka ya serikali kwa hiyo sisi hatuna sababu ya kukihoji.

    3. Si kila paspoti inatolewa baada ya kuonyesha cheti. Hata afidaviti inakubalika.

    4. Hayo makopi ya leseni na paspoti yaliyoko mtandaoni hayakubaliki kuwa ushahidi wa aina yeyote kwenye mahakama yeyote kwa sababu ya photoshop. hivyo hatupotezi muda kuyapa nafasi.

    5. Kila mtu ni mwema mpaka uthibitishe ukosefu wake. Ni kazi ya watuhumu kuthibitisha kuwa tuhuma zao ni za kweli kwa kiwango cha kuzidi kivuli cha mashaka. Na si kazi ya mtuhumiwa kuthibitisha kuwa yeye ni msafi bali kwa uwezekano tuu kuwa tuhuma ni za uongo.

    6. Kuwepo wagushi wengi polisi na jeshi si utetezi bali "AMBAYE HAJAZINI AWE WA KWANZA KUMPONDA JIWE." Kama wagushi wa leo wakiadhibiwa na wale waliko makazini nao waadhibiwe. Hii ni kama ni waadilifu na watenda haki.

    Hashim ungechukuwa vikozi vya sheria hapa kulikuwa hakuna hoja. Uzito wa hoja za watuhumu unakuja na udhaifu wa watuhumiwa.

    ReplyDelete
  5. Hashim kasema ukweli (unauma), watu bado si wastaarabu na anatarajia zaidi ya hayo. Kutostaarabika kunaashiriwa na mienendo ya kila siku
    1. Kutpa taka ovyo
    2. Ufisadi,
    3. Rushwa,
    4. Lugha chafu,
    5. Shule na vyuo vya kata (hakuna kujenga fikira)
    6. Imani ya ajali haina kinga
    7. Kuheshimu privacy
    8. nk.

    ReplyDelete
  6. Ushauri mdogo tu kwa Lundenga, sasa hivi dunia ni kijiji. Watu wanauthibitisho wa umri wa Siti. Kama wewe unadai yupo sahihi basi ina maana mwakani hatuna mwakilishi wa Ms. World Tanzania. Maana watu wameamua kulifikisha swala hili katika ngazi ya kamati ya Ms. World. Maana Tanzania tarehe ya kuzaliwa unaamua tu unavyojisiskia. Hatukubali mwakilishi mwongo kwenye ngazi ya kimataifa. Hii ni case ya udanganyifu, nashangaa kwanini mpaka leo hatua hazichukuliwe. Ushiriki utaishia kwenye ngazi za Taifa, mpaka mkunga aliyemzalisha mama yake atakuja kusaidia ushahidi kama mama yake anajitoa ufahamu.

    ReplyDelete
  7. MHESHIMIWA LUNDE, KUMBUKA VILE VISA ULIVYOFANYA KIPINDI KILE MELI ILIPOZAMA ZANZIBAR?
    UNAKUMBUKA ULIJIBU NINI ULIPOSHUTUMIWA?
    SASA MAMBO NDIO MAMBO YANAKURUDIA. SI KITAMBO HII ISSUE YA MISS TANZANIA ITAKWENDA NA MAJI. UMESHACHAKACHUA VYA KUTOSHA LAKINI ZA MWIZI AROBAINI.
    TENA UJICHUNGE SANA NA KAULI ZAKO DHIDI YA POLISI VINGINEVYO WANAWEZA KUKUZUSHIA VARANGATI USIJUE PA KUKIMBILIA

    ReplyDelete
  8. Jamani si nasikia kaachia taji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...