Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Saba wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, yamekamilika ambapo mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 700 toka nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Eliud Sanga, amesema maadalizi yote ya mkutano huo, wenye kauli mbiu ya "Maadhimisho ya Miaka 70 ya Ukuaji na Huduma Bora, LAPF", yamekamilika ambapo utakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF.

Bwana Sanga amesema Mfuko wa LAPF  ndio mfuko unaoongoza sii tuu kwa kutoa mafao bora, bali pia ndio mfuko unaoongoza kwa kuwa na afya bora kabisa ambapo kwa sasa una rasilimali zenye thamani ya shilingi bilioni 700, LAPF ndio mfuko unaoongoza kukua kwa kasi zaidi ambapo unakuwa kwa asilimia 21 kwa mwaka!.

Ameendelea kutoa sifa za LAPF kuwa ni pamoja na kuwa ndio mfuko unaolipa kwa haraka zaidi, ambapo mstafuu kama anastaafu kesho, LAPF wao wanalipa jana!.

Bwana Sanga hakuishia hapo, amesema LAPF ndio mfuko unaoongoza kwa utunzani wa mahesabu kati ya mifuko yote kwa mujibu wa NBAA, na ndio mfuko unaokuwa kwa kasi zaidi kwa mujibu wa SSRA!.

Mkutano huo, utafunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Ghasia, na Kufungwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Eliud Sanga, akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe, kushoto kabisa ni Meneja Takwimu, Tathmini na Hadhari wa LAPFBw. Aboubakar Ndwata.Kulia ni Meneja wa LAPF Kanda ya Kaskazini, Rajabu Kinande.
Meneja Kanda ya Dar es Salaam wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Amina Kassim akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe na Kulia ni Meneja wa LAPF Kanda ya Kaskazini. Rajabu Kinande.
Meneja Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Rajabu Kinande, akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Amina Kassim, na Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...