DSC_0216
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano kati ya nchi ya yake na Umoja wa Mataifa ambapo wametoa fedha kusaidia miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye ofisi za ubalozi wa Sweden jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha na Zainul Mzige).

Na Mwandishi wetu
SWEDEN imeyapatia mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini jumla ya shilingi bilioni 42/- ili kusaidia katika miradi yake ya maendeleo inayofanya nchiini Tanzania.
Makubaliano ya fedha hizo yametiwa saini jana kati ya Balozi wa Sweden Lennarth Hjelmaker na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez.

Fedha hizo ambazo ni sawa na dola milioni 24, zitaelekezwa kwenye miradi ya UNDAP inayoendana na sera za Sweden za kuwezesha masuala ya utawala bora, ustawi wa jamii, wanawake na watoto na usawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Balozi wa Sweden, fedha hizo zitasaidia utekelezaji wa Mkukuta, Mkuza na Matokeo makubwa sasa (BRN) mipango inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa .

Alisema ni matumaini yake kuwa fedha hizo zitaboresha hali ya kufanya biashara, kuwekeza kwa lengo la kutoa ajira zaidi,kuwezesha uchaguzi huru, kuimarisha huduma za jamii, kuimarisha mipango, uwajibikaji na kuimarisha mawasiliano ya radio kwa ajili ya upashanaji habari vijijini ili kusaidia maamuzi yenye mtazamo mpana zaidi miongoni mwa watu wa vijijini.
IMG_2231
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakitiliana saini makubaliano ya msaada wa fedha hizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za ubalozi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...