MAKATIBU WAKUU WA WIZARA

 Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha mmoja, uteuzi uliomuondoa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Charles Pallangyo.
Pallangyo sasa anakua Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, nafasi ambayo inatafsriwa kuwa adhabu, siku chache baada ya vyombo vya habari ikiwamo FikraPevu kuibua kashfa ya uhaba wa dawa katika hospitali kubwa za serikali.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa ni pamoja na Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuchukua nafasi ya Pallangyo.

Katika uteuzi huo Dkt. Yohana Budeba anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba amepanda na kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro anahamishiwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA kuchukua nafasi ya Dkt. Meru.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Niliandika hapa hapa siku Pallangyo alivyoteuliwa kuwa katibu mkuu wizara ya afya...this guy he is a "general" economist...and you can't have wizara ya afya led by just an economist.

    Leo naandika tena, I don't think Dr Mmbando also fits to that position.

    Where are the "health economists" or "health systems specialists" in Tanzania. We have many of them, why are we not giving them such positions.

    Tuta-recycle mpaka basi....

    ReplyDelete
  2. Mh. Rais pia atuchugulie nasi Chuo cha Ustawi tuko chini ya wizara ya afya ni majanga watumishi tuko hoi tunateseka hiki chuo hakina serikali jamani idara zote zimeshikwa na kabila moja ambaye ni ya huo kiongozi tunalia tunakufa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...