MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Kambangwa,Denis Casmiry mwenye umri wa miaka 16 (pichani) amekutwa kwenye ufukwe wa Salander Bridge akiwa amefariki dunia

Akizungumza na Ripota wetu huku akionekana kuwa na masikitiko makubwa,Baba Mzazi wa Mtoto huyo aliejitambulisha kwa jina la Casmiry,amesema kuwa walipata taarifa ya mtoto wao kupotea toka Jumamosi Desemba 20,2014 ambapo inadaiwa kuwa aliondoka nyumbani kwao akiwa na marafiki zake kwenda kwenye Mazoezi ya viungo kwenye ufukwe huo wa Coco Beach.

"Aliondoka hapa nyumbani asubuhi na mapema kwenda kwenye mazoezi akiwa na wenzake,na walipomaliza kufanya mazoezi yao hayo,waliamua kuogelea kidogo ikiwa ni kawaida yao kila wanapomaliza mazoezi wanafanya hivyo,mara baada ya kumaliza kuogolea wenzake walitoka kwenye maji na hapo ndipo walipobaini kuwa mwenzao hawakuwa nae" alisema Bw. Casmiry.

Aliendelea kusema kuwa "Baada ya kufanya juhudi za kumtafuta mwenzao bila mafanikio,vijana hao walirudi nyumbani na kutupatia taarifa na sisi bila kuchelewa tulitoa taarifa kituo cha Polisi na kutoa na askari wachache mpaka eneo la tukio na pia hatukuweza kumuona mpaka leo hii tunaukuta mwili wake Ufukweni,inauma sana kwa kweli".

Mwili ya kijana huyo umekutwa kwenye ufukwe ya Salander Bridge,Jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi waliokuwepo kwenye eneo la tukio wakijadiliana jambo wakati wakijiandaa kwenda kuuhifadhi mwili wa kijana huyo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa. Jamani basi binadamu hata akifa utu wake uheshimiwe. Mbona hajasitiriwa? Hata kama ni polisi ni makosa kubeba maiti ikiwa haijahifadhiwa (kusitiriwa) Inauma sana kuona binadamu anabebwa ktk machela namna hii.

    ReplyDelete
  2. Bongoland tunabeba hivyo, na ilitakiwa abebwe na Polisi in a humane way. I doubt if they do any postmortems, hao wangevaa goloves so that wasiharibu ushahidi, inwezekana aliuwawa na kutupwa baharini. Poleni wafiwa.

    ReplyDelete
  3. Hivi Coco Beach bado haina lifeguards? Nafikiri kuwa na lifeguards beach zote ndio suluhisho la kuokoa maisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...