DSC_0013
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,na Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh. Aggrey Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi karibuni katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC).

Na Mwandishi wetu, Arusha
MTAALAMU mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, ameishauri serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa wananchi wake.

Dhliwayo alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi wa jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii kwa wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka 2025 ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.

Dk. Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa na Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini Zimbabwe na Msumbiji.

Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.
DSC_0005
Ofisa anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi. Usha Mishra akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na kutoa mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...