Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.

Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Crencencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport Financial Services mkoani Mwanza.

Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.

Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau, hususan wale wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia ulinzi wa kutosha.

Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino.
Mbunge wa kuteuliwa Mh. Shaimar Kweigyir katikati akiwa na bibi wa Yohana Bahati (Tabu Maganiko) kulia ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha. Kushoto kwake ni Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari.
Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbunge naona unakazi nzito yakuffanya sio kutembea kwenye vx yako ndugu zetu wanahitaji msaada mkubwa sio unajifanya kwenda kufariji baada ya tukio.kikosi maalum cha usalama wa taifa wapewe hii kazii na watakaobainika hasipelekwe kwenye vyombo vya sheria waangamizwe hii ndio dawa ya watu hao

    ReplyDelete
  2. Ninapata wakati mgumu kuhusu sincerity ya serikali kwenye swala hili ambalo limekuwa likijirudia x2 kila kukicha.Swali langu kubwa ni kwamba, ni kweli serikali kupitia vyombo vyake vyote vya kiusalama wameshindwa kuzuia kabisa mauwaji haya ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi? Wakati common sense inaonyesha dhahiri kuwa the common denominators wa shughuli hii ni waganga wa kienyeji (wachache).sasa ugumu wa kuwapata wadau wa hii biashara haramu na kuikosesha unatoka wapi?

    ReplyDelete
  3. OMBI: Michuzi mpelekee salamu Shigongo kuwa hizo harakati zake za kufichua maovu katika jamii azielekeze katika kufumua mtandao wa wauwaji hawa kuliko kutuletea hadithi za wafanya ngono.jambo ambalo jamii inacare the least.Lakini hili la Albino licha ya kuwa ni unyama usio vumilika vilex2 ni aibu kubwa kwa taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...