Mwamuzi wa Mpambano wa Masumbwi uliowakutanisha mabondia Mohamed Matumla (Tanzania) na Wang Xin Hua (China) katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam usiku huu,akiwa amemnyanyua mkono Bondia Mohamed Matumla baada ya kumchapa kwa Point bondia mwenzake kutoka nchini China katika mpambano wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka mwezi Mei mwaka huu, huko nchini Marekani.
Wanahabari wakichukua taswira mbali mbali za mpambano huo.
Bondia Mohamed Matumla akiangalia namna ya kumrushia konde mpinzani wake Wang Xin Hua (China) wakati wa mpambano wao wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka mwezi Mei mwaka huu, huko nchini Marekani.Katika Mpambano huu, Bondia Mohamed Matumla alishinda kwa point.
Matumla akimchezesha Wang Xin Hua.
Wang Xin Hua akirusha konde kwa Mohamed Matumla ambaye leo alikuwa makini sana kuhakikisha hampi point hata moja mpinzani wake.
Matumla anatakata hapa,anampa ambakati moja maridadi kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...