Na. Anitha Jonas na Johary Kachwamba -MAELEZO, DODOMA

WAZIRI wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka amesoma Muswada wa Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini wa mwaka 2014 kwa mara ya pili ikiwa muswada huu umelenga masuala mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi pamoja na mahitaji ya kiteknolojia ambayo ni kichocheo kikubwa  cha uhamiaji wa nguvu kazi kutoka nchi moja kwenda nyingine.

 Mhe.Kabaka alisema kwa sasa zipo mamlaka nyingi zinzotoa vibali vya ajira kwa wageni kwa kuzingatia sheria zinazosimamia maswala ya Uhamiaji, Uwekezaji, Elimu, Biashara na Wakimbizi, hivyo hali hii ya kuwepo na mamlaka nyingi zinachangia  kusababisha usumbufu kwa wawekezaji na kokosekana kwa uwajibikaji pamoja na kuwepo na udanganyifu.

“Kutungwa kwa sheria hii kunalenga kutelekeza kwa manufaa ya nchi yetu mikataba ya kikanda inayoruhusu uhamiaji huru wa nguvu kazi hususani inayohusu itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afika Mashariki na Ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika SADC” alisema Mhe. Kabaka.

Katika kutekeleza mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu uhamiaji na nguvu kazi, utaratibu wa kutoa vibali vya ajira kwa wageni umekuwa ukitumika ili kuhakikisha nguvu kazi ya wageni hao inaleta manufaa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na pia katika kulinda ajira za wananchi.

Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Mhe.Celina Paresso Mbuge wa Viti Maalum-CHADEMA aliishauri Wizara ya Kazi na Ajira kushirikiana na wizara mtambuka kama Wizara ya Viwanda na Biashara na Idara ya Uhamiaji, kufanya ukaguzi wa vibali vya ajira hasa katika maeneo ambayo raia wa kigeni wanafanya shughuri zao bila kuzingatia sheria za nchi.

“Tanzania tuna maliasili nyingi, lakini dunia ya leo na ijayo itatawaliwa na wenye maarifa, kwa maana ya sayansi, teknolojia, elimu na ujuzi” alisema Mhe. Paresso

“kuwa na maliasili peke yake haitoshi, hatuna budi tujinoe kwa elimu na ujuzi, na hasa elimu inayomuwezesha mtu aajirike au ajiajiri” aliongezea Mhe. Paresso

Endapo Mhe. Rais ataridhia, Sheria hii itaanza kutumika tarehe 1 Julai, 2015. Kutungwa na kuanza kutumika kwa Sheria ya Ajira ya Wageni Nchini kutakuwa na matokea chanya ikiwema uratibu mzuri wa ajira za wageni nchini, kuongezeka kwa ajira za watanzania na kuongezeka kwa ujuzi kwa wafanyakazi wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...