Na Chalila Kibuda 

Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu amewataka watu wajitokeze katika  harakati za kupambana na watu wenye imani  potofu za kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Mdimu amesema uchunguzi umebaini ukosefu wa elimu kwa watu wenye imani hizo ndiyo hupelekea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo silaha ya elimu ni sehemu kubwa ya harakati hapa nchini.

Hayo ameyasema leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kusema kuwa ana mpango wa kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Aidha,Mdimu ameahidi kutoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa kwa kuwatumia baadhi ya wasanii kama Jhikoman,Kassim Mganga,Profesa J,Ray C,Fid Q,Roma Mkatoliki pamoja na Dami Msimamo.

Pia amevitaka Vyombo vya Habari kutoa ushirikiano katika harakati hizo za  kuhakikisha wanatokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
 Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu (kati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati azungumzia harakati zake za kutaka kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mwenyekiti wa Imetosha Movment,Masoud Ali "Kipanya" na kushoto ni Monica Joseph mjumbe wa Imetosha.
 Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni Wajumbe wa Imetosha,Joachim Mushi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa Imetosha wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...