Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto) akimsalimia mtumishi wa Wizara hiyo, Said Ngovi ambaye ni mvuta kamba wa timu ya Utawala wakati Mkurugenzi huyo alipokuwa anazikagua timu mbalimbali za wizara hiyo katika Tamasha la Michezo la kwanza lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kapteni wa timu ya wanaume (Utawala) ya kuvuta kamba, Ally Lubuva.
 
 Kapteni wa Timu ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Chilipweli (kushoto) akiimasisha timu yake kuivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu hizo zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
 
 Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mary Nyegazeni akiishangilia timu yake ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume baada ya kunyakua pointi mbili kwa kuivuta timu ya Uhamiaji katika mashindano maalumu ya Tamasha la Michezo la wizara hiyo ambalo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...