Waziri wa Ujenzi Dkt ,John Magufuli akizungumza na wakandarasi kutoka kampuni ya Dot Services ya nchini Uganda inayo jenga barabara ya Korogwe/Mkumbara hadi Same. |
Waziri wa Ujenzi Dkt Magufuli akizungumza jambo wakati alipokutana na watenadji wakuu wa kampuni ya Dot Services wanaojenga barabara ya Korogwe/Mkumbara hadi Same. |
Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SERIKALI imetaka wakandarasi wa barabara nchini, kutekeleza miradi ya barabara
kwa wakati na ubora unaokubalika ili kuwaonesha wahisani namna ambavyo fedha wanazotoa
zinafanya kazi iliyokusudiwa kwa kuonesha thamani halisi ya mradi husika.
Hayo yalielezwa juzi na waziri wa Ujenzi, Dkt John Magufuli wakati akifanya
ukaguzi wa barabara kutoka Korogwe/Mkumbara hadi Same yenyeurefu wa Kilomita 172,inayojengwa kwa fedha za
mkopo kutoka benki ya
dunia (WB).
Dkt Magufuli alisema changamoto mbalimbali zinazojitokeza
katika ujenzi wa barabara hazina budi kutafutiwa
ufumbuzi wa mapema, ili kutoa nafasi kwa rais Jakaya Kikwete kuifungua na kuruhusu
wananchi kuendeleza shughuli za uzalishaji mali.
Alisema katika kuhakikisha barabara hizo zinadumu ni vyema kwa Tanroad
kutafuta mizani inayohamishika (Mkeka) ili kuwadhibiti
wasafirishaji wasio
waaminifu ambao wamekuwa wakibeba mizigo mikubwa kwa tamaa ya fedha.
" Kukamilika kwa barabara hizi kutarahisisha shughuli za kiuchumi
kwa mikoa hii inayopitika ,Nikuombe katibu mkuu kwa kushirikiana na wahandisi, kuhakikisha hizi Bil 200 ambazo ni mkopo
hazipotei, nataka mdhibiti magari yanayobeba mizigo mikubwa....wakati fulani
tulishika magari yenye uzito wa Tani 96 hadi 102, uzito unaokubalika kisheria
ni
Tani 56 tu"alisema Magufuli..
Naye mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mhandisi Partick
Mfugale alimweleza Wazri Magufuli kuwa barabara ya kutoka Korogwe/Mkumbara
hadi Same yenye urefu wa Kilomita 172 inajengwa kwa
awamu mbili tofauti.
Alisema barabara hiyo ambayo sehemu ya barabara inatoka Dar es
salaam ,Chalinze,Arusha hadi Nairobi, imegawanywa mara mbili, Korogwe/Mkumbara
Km 76 kinachojengwa na kampuni ya Strabag ya Ujerumani na Mkumbara/Same
Km 96 inajengwa na kampuni ya Dott services ya Uganda.
Mfugale alisema ujenzi wa kipande cha Korogwe/Mkumbara
ulianza Mei,2012 na kumaliza Desemba 3,2014 na uligharimu Bil sh 87.805 kwa
mkandarasi na kiasi cha Sh Bil 6.787 kwa mhandisi msimamizi kampuni ya Nicholas
O'Dwyer Ltd ya nchini Ireland kwa miradi yote miwili.
Alisema Kazi alizofanya katika mradi huo ni kubandua na kusaga lami iliyokuwepo
na kuweka lami nyingine mpya kwa mfumo imara zaidi,kuimarisha daraja la Mombo,
kujenga makalvati makubwa 18 na madogo 175 na sasa kazi imekamilika na
yupo katika muda wa uangalizi.
Mradi wa pili ni Mkumbara/Same Km 96 wenye gharama ya Bil 103.8kupitia
mkandarasi wa Dott services ya Uganda ambao walikubwa na changamoto kadhaa
ambazo sasa zimerekebishwa na sasa ameanza ujenzi kwa kasi.
Alisema makubaliano ni kujenga angalau Km 4 kwa kila mwezi ambapo sasa amekamilisha
asilimia 67 ya mradi husika na matarajio ni kukamilishamradi wote hadi kufikia
muda wa mkataba ambao ni Disemba mwaka huu.
Mfugale alisema mkandarasi huyo tayari amelipwa kiasi cha Sh Bil 44.5na
kazi inaendelea vizuri ingawa alitaka mkandarasi huyo kuhakikisha kasi ya
ujenzi anayofanya sasa ilingane na ubora wa barabara inayojengwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...