Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Jumla ya Pikipiki 10 zenye thamani ya Sh.Million 42 zimegawiwa kwa Maafisa 10 wa Afya wa Wilaya za Unguja na Pemba. Pikipiki hizo ni Msaada kutoka Shirika la Watu wa Marekani USAID kupitia Taasisi ya JSI wenye lengo la kusaidia Sekta ya Afya Zanzibar. 
 Akikabidhi Pikipiki hizo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amewataka Maafisa Waliokabidhiwa kuzitumia vyema ili kutimiza lengo lililokusudiwa. Amesema ana imani kubwa kuwa zitasaidia kwa kiasi kikubwa Usimamizi na usambazaji mzuri wa Dawa katika kila Wilaya ya Zanzibar. 
 "Kwa kweli pamoja na kuwashukuru Wahisani wetu USAID na JSI tunaamini sasa Usimamizi na Usambazaji wa Dawa utakuwa bora na kwa wakati maana Pikipiki hizo ni usafiri wa Rahisi" Alisema Naibu Mahmoud. 
 Amewataka Maafisa hao kutoishia kusambaza Dawa tu bali wapitie kila kituo cha Afya kutafuta Matatizo na kuyaripoti Sehemu husika ili yaweze kushughulikiwa. 
 Aidha Naibu Mahmoud amewashauri Viongozi wa Wizara ya Afya kutoa Motisha kwa Watendaji wanaoweza kukabidhiwa Vitendea kazi na kuvitunza vyema. Kwa upande wao Maafisa waliokabidhiwa Pikipiki hizo wameishukuru Serikali kwa Juhudi zake za kutafuta mbinu mbali mbali za kukabiliana na Changamoto na kuzifanyia kazi. 
 Mmoja wa Maafisa hao Mayasa Othman Shariff kutoka Wilaya ya Chake Chake amesema Pikipiki hizo zitawarahisishia kazi zao ikiwa ni pamoja na kusambaza na kusimamia Dawa sambamba na kupeleka Ripoti mbali mbali sehemu husika. Mfamasia Mkuu Dkt. Habib Ali Shariff alisema miongoni mwa Changamoto zinazokabili Sekta ya Afya ni pamoja na Usimamizi mbaya wa Dawa hivyo Pikipiki hizo zitasaidia kupambana na Changamoto hiyo. 
 Hafla ya Kukabidhiwa Pikipiki hizo ilifanyika katika Viwanja vya Bohari kuu ya Madawa Maruhubi Zanzibar ambapo Wilaya zote 10 za Unguja na Pemba zilipatiwa Pikipiki moja na kukabidhiwa Maafisa wa Afya wa Wilaya husika. Wizara ya Afya imekuwa ikifanya Juhudi mbali mbali za kukabiliana na Changamoto za Sekta ya Afya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kutafuta Wafadhili kutoka Nchi tofauti ambapo Shirika la Watu wa Marekani USAID ni mdau muhimu wa kusaidia Sekta hiyo Zanzibar.
 Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Dkt. Habib Ali Sharif akizungumza na Mafisa wa Afya wa Wilaya kabla ya kukabidhiwa Pikipiki kwaajili ya usambazaji wa Dawa Wilayani, pikipiki hizo zimetolewa na Shirika la watu wa Marekani (USAID) hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika Bohari Kuu la Madawa Maruhubi Mjini Zanzibar. 
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) akimkabidhi Pikipiki Afisa wa Afya wa Wilaya Nd. Khamis Daud Ali katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Maruhubi.
 Mafisa wa Afya wa Wilaya wakiwa kwenye Pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa.

Mafisa wa Afya wa Wilaya wakiwa kwenye Pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...