Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
JAMII imeaswa kutumia elimu sahihi ya matumizi ya vyandarua katika kuweza kupambana na ugonjwa wa malaria.

Hayo ameyasema leo Kaimu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John wakati akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,amesema jamii imetakiwa kutumia elimu sahihi katika kupambana na malaria.

Amesema malaria imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2012 na kufikia asilimia 10 mwaka huu hiyo imetokana na juhudi za wizara ya afya na mashirika mbalimbali kutoa elimu juu kujikinga ugonjwa huo ambao awali ulikuwa ikichangia vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutokana na kutokana na kukosa vyandarua.

John amesema katika madhimisho ya siku ya malaria ambayo itaadhimishiwa jijini Dar es Salaam yatakwenda sambamba na uzinduzi  wa ugawaji wa vyandarua milioni 24 vilivyotolewa na Wizara ya Afya ikiwa lengo kupambana na ugonjwa wa malaria. Amesema mikoa ambayo iko katika viwango vya juu vya ugonjwa wa Malaria ,Lindi,Geita ,Kigoma pamoja na Mara hali ambayo elimu inahitajika kwa mikoa hiyo katika matumizi sahihi ya vyandarua  kuweza kufikia asilimia sifuri.

John amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Maralia ni Wekeza kwa Maisha ya Baadae ,Tokomeza Malaria na maadhimisho hayo itatumika sehemu ya kuelimisha juu ya kutambua dalili za malaria kuwahi katika kituo cha kutolea huduma,ili kupima na kudhibitisha uwepo wa vimelea kabla ya kuanza kutumia dawa kwa kuwa sio kila homa inasababishwa na Malaria.
 KAIMU Katibu Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John akiandika maswali aliyeulizwa na waandisshi wa habari (hawapo pichani ) juu ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani  -Tanzania ,Dk.Ritha Njau ,Kulia ni Naibu Mkurugezi Kituo cha Utafiti cha Ifakara,Dk.Abdulrazq Badru.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,Kushoto ni  Naibu Mkurugezi Kituo cha Utafiti cha Ifakara (IHI),Dk.Abdulrazq Badru.
 Meneja wa Mpango wa Kudhibiti Malaria wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,DK.Ben Mandike akisisitiza jambo  kwa waandishi  habari juu ya maadhimisho  ya siku ya malaria Duniania  iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.
Watalaam na watafiti wa malaria wakifatilia mada mbalimbali katika mkutano wa tano wa taarifa ya miaka mitano ya utafiti wa Malaria na hali halisi ya sasa iliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti cha Ifakara na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hatutendi haki kuongelea vyandarua tu wakati hoja ya msingi ya mbinu za kutokomeza mmbu kama vile kurejesha matumizi ya DDT ambayo wakubwa duniani baada ya kumaliza mbu kwao wakaipiga marufuku nasi tukaunga bogi kama wendawazimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...