Na Bashir Yakub.
Katika migogoro ya ardhi yapo mambo mengi ambayo hujitokeza. Yumkini hii yote huwa ni katika kusaka haki. Liko jambo moja ambalo ni muhimu watu kulijua hasa wale ambao tayari wamejikuta katika migogoro ya ardhi. Mara nyingi imekuwa ikitokea pale ambapo mtu fulani ana mgogoro wa ardhi na mtu mwingine kumwendea polisi na kumshitaki kwa jinai ya kuvamia ardhi yake( criminal trespass). Ni kweli jambo hili lipo kisheria lakini haliko moja kwa moja kama ambavyo watu wamekuwa wakilichukulia kama ambavyo tutaona badae.
1.JINAI YA UVAMIZI WA ARDHI.
Nimesema hapo juu kuwa jinai ya uvamizi wa ardhi huitwa “criminal trespass”. Kosa hili huhesabika limetendeka pale ambapo mtu huingia katika ardhi ya mtu mwingine bila ruhusa au mamlaka yoyote ya kisheria kutoka kwa mmiliki au penginepo huku akiwa na nia mbaya. Mtu anapokuwa amefanya hivi tayari huhesabika ametenda jinai ya uvamizi wa ardhi. Ardhi kwa maana hii hapa hujumuisha nyumba, shamba, kiwanja na kila kitu ambacho huitwa ardhi.
2. KESI YA MADAI YA UVAMIZI ARDHI.
Hapo juu nimeeleza kosa hili la uvamizi ardhi lakini katika upande wa jinai. Yafaa tujue kuwa kosa hili pia ni madai. Kwa hiyo kama hapo juu tumeona anayevamia ardhi ya mtu anaweza kufunguliwa kesi ya jinai basi tuelewe kuwa kwa kosa hilohilo waweza fungua pia kesi ya madai. Tofauti ya kesi ya madai na jinai katika kosa hili ni kuwa katika kesi ya jinai mtuhumiwa akipatikana na hatia basi atatakiwa kwenda jela au adhabu nyingineyo wakati katika kesi ya madai mlalamikiwa akipatikana na hatia basi atatakiwa kulipa fidia kwa mtendewa. Kwa hiyo uamuzi wa kesi gani mlalamikaji afungue uko mikononi mwake. Aidha yawezekana pia kufungua kesi zote mbili kwa pamoja yaani mahakama fulani ukafungua kesi ya madai na mahakama nyingine ukafungua kesi ya jinai kwa wakati mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...